AVRAM
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 616
- 885
Ni muda mrefu umepita watanzania wanaoishi nje ya nchi yao (Tanzanian Diaspora) wamekuwa wakizungumza na kupigia chapua kwa nguvu suala la sheria ya uraia pacha; yaani uraia wa nchi mbili "Dual citizenship", kwa upana na wasaa zaidi suala hili tayari limejadiliwa na kutolewa uchambuzi wa kutosha juu ya faida na hasara zake kwa nchi endapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakubali au kukataa kuanzisha sheria ya uraia pacha.
Kadhalika; katika kuwapa moyo, kila wakati viongozi wa kitaifa wanapojaaliwa fursa ya kuwatembelea wanadiaspora katika nchi wanazoishi na kufanya kazi, huwa wanalitolea ahadi nzuri nzuri suala hili kwamba; Mamlaka zinazohusika zinatafuta utaratibu mbadala unaofaa zaidi kando na sheria ya uraia pacha, utakao toa hadhi maalum kwa wanadiaspora wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania endapo suala la uraia pacha litaonekana na kuthibitika kuwa halina faida na usalama kwa taifa letu kiuchumi na kijamii.
Sasa ni muda muafaka kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuharakisha utaratibu maalum wa kufuatwa ili Tanzania kunufaika na Wanadiaspora wake, na wanadiaspora kufaidika na fursa zinaonekana hapa Tanzania.
Mamlaka zinazowajibika na jambo hili, zinapaswa kuandaa utaratibu mzuri wa kufuatwa ambao Tanzania inaweza kuutumia ili kukidhi mahitaji ya Diaspora kwa kuwapa hadhi maalum na hatimae kuwanufaisha bila ya kuwepo Sheria ya Uraia wa Nchi mbili kwa kuiga mifano na taratibu zinazotumika katika nchi za Ethiopia, India, Indonesia na kwengineko.
Kwa bahati, wakati najaribu kupanga mawazo vizuri, nimefanikiwa kupitia taarifa za baadhi ya nchi zenye utaratibu mzuri wa namna hii, ambapo Tanzania tunaweza kuiga utaratibu huo kwa kurekebisha kulingana na mahitaji yetu. Hapa zaidi nimetolea mfano kwa nchi ya Ethiopia na India.
Kama sikosei, kulingana na katiba ya Ethiopia, uraia pacha hauruhusiwi, kwa iyo Diaspora wote wa Ethiopia walioukana ama kuuacha uraia wa nchi yao, wamepata sifa ya kushiriki katika masuala yote ya kijamii na kiuchumi isipokuwa ya kisiasa, kupitia tangazo rasmi na kanuni (Proclamation No. 101/2004), ambazo kanuni hizi ziliweka utaratibu wa kisheria wa waethiopia wanaoishi ughaibuni kupata kadi za uraia wa Ethiopia (Ethiopia origin ID Card), maarufu kama “YELLOW CARD”.
“YELLOW CARD” lengo mtawalia la kadi hii ni kutoa fursa kwa wanadiaspora wa Ethiopia kupata haki za kisheria kushiriki katika masuala ya kiuchumi na kijamii kwa kuwaondolea vikwazo vya kisheria. Kadi hii inampatia Diaspora wa Ethiopia haki zifuatazo:-
a) Kuingia Ethiopia bila ya visa
b) Kupata ajira bila ya kibali cha kazi
c) Kushiriki katika taratibu ya mafao ya uzeeni,
d) Watoto kuwa na haki sawa na mzazi mwenye kadi hiyo.
Lakini, vilevile taamko hili halikuacha kuoneaha wazi fursa atakazozikosa mwanadiaspora huyu ambae atakuwa na kadi hiyo, yaani Yellow Card, ambazo ni:-
a) Kutoshiriki kwenye masuala ya kisiasa; kwa maana ya uchaguzi katika ngazi zote, Hapa nakusudia kuchagua ama kuchaguliwa katika ngazi zote za uchaguzi, kuanzia mwanzo vijijini hadi ngazi za kitaifa.
b) Hawezi kupata ajira, yaani kufanya kazi katika vyombo vya ulinzi na usalama pamija na swhemu zote nyeti kwa usalama wa taifa; Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na Wizara ya mambo ya Nje.
Serikali ya india kupitia mabadiliko ya kisheria “The Citizenship (Amendment) Act” ya mwaka 2005, iliwatambua na kuwapa raia wenye asili ya India ambao wana uraia wa nchi nyengine hadhi ya kiraia iliyopewa jina la ubatizo la “Overseas Citizenship of India – OCI”.
Utaratibu huu ulianzishwa ili kujibu hoja na malalamiko ya muda mrefu ya kuwa na uraia wa nchi mbili yaliyokuwa yakitolewa na Wanadiaspora wa India waliokuwa wakiishi katika nchi zilizoendelea. Ili kutatua kero hiyo Serikali ya India iliunda Kamati Maalum ya Diaspora iliyokaa na kujadili na baadae kuleta mapendekezo ya kufanya marekebisho ya Sheria ya Uraia ya India. Hatimae; kupitia mabadiliko hayo ya mwaka 2005. India ilianzisha hadhi hiyo ya kiraia na kuanza kutoa kadi za OCI.
Kwa kuwa katiba ya India hairuhusu Raia wake kuwa na uraia wa nchi mbili; hivyo mhindi mwenye kadi hii “OCI Cardholder” hatakiwi kuwa na pasi ya kusafiria ya India akiwa bado ana uraia wa nchi nyengine (isipokuwa raia wanaoishi katika eneo la Jammu na Kashmir; ambapo yanaeleweka na Umoja wa Mataifa kuwa yana mgogoro).
Kadhalika; Mmiliki wa kadi hii anakuwa sio raia wa India isipokuwa ana haki na kuruhusiwa kuishi na kufanya kazi katika Jamhuri ya India katika muda wote wa maisha yake bila ya kikomo.
Kwa mfano uleule wa Ethiopia hapa chini nimeainisha haki anazozipata Mhindi mwenye kadi ya OCI:-
a) Kuingia na kutoka nchini India wakati wowote bila ya kuhitaji kibali au viza,
b) Kutotakiwa kujiandikisha katika ofisi za Uhamiaji kila anapoamua kukaa nchini India kwa muda mrefu, na
c) Kushirikiana na Raia wasiowakaazi wa India katika masuala ya kiuchumi, kifedha na kielimu.
Mabadiliko ya sheria pia yalionesha haki anazozikosa Mmiliki wa OCI kama ifuatavyo:-
a) Haki ya kupiga kura,
b) Haki ya kuchaguliwa kushika nafasi ya uongozi kikatiba kama vile Ubunge, Urais, makamu wa Rais na Jaji wa Mahkama kuu,
c) Haki ya kununua ardhi kwa ajili ya kilimo, na
d) Haki ya kuajiriwa serikalini.
Baada ya kupitia na kusikiliza mijadala kadha ya wanadiaspora wa Tanzania, hapa chini nimeainisha baadhi ya changamoto zinazowapata wanadiaspora:-
1. Umiliki wa ardhi na mali zisizohamishika,
2. Changamoto zinazowapata wakati kuingia, kuishi na kutoka nchini. Sheria hii inawaona wanadiaspora hawa sawa na raia wengine wa kigeni. (Sheria ya uraia na uhamiaji kwa hivi sasa inawalazimisha kulipia viza, na vibali vyengine vinavyostahiki kulingana na malengo ya mwanadiaspora).
3. Urithi wa mali na mitaji ya kibiashara ama uwekezaji.
4. kushiriki katika siasa, hapa ikijumuisha kupiga kura, kuchagua ama kuchaguliwa katika ngazi zote za uchaguzi.
Kuna baadhi ya wanadiaspora katika mijadala mbalimbali, huwa wanaonesha nia thabiti ya kutaka kushiriki katika ujenzi wa nchi yao ya awali, ama kwa kutoa misaada, kuekeza mitaji ya kibiashara au kushiriki katika kutoa utaalamu wao, ila sheria za uhamiaji na uraia zinakuwa kikwazo kwao kiasi kufikia kukata tamaa na kuweka kando mawazo chanya walionayo kwa nchi yao.
Tunafahamu kuwa kila binaadamu kiasili ana kwao, na nafsi ama moyo wa binaadamu yoyote mwenye kwao hautaacha kutamani kwao, kwaiyo hata tuone mtu ameishi UK miaka 40 ama 50 hata acha kuhisi utanzania wake, hapa ndio tunakuja kufahamu kuwa mtu kuchukua uraia wa nchi nyengine sio kwamba anapenda sanaaaaa ila kinachotokea ni kurahisisha upatikanaji wa fursa ambazo sheria za nchi uliopo hazikuruhusu kunufaika nazo hadi uwe raia wa nchi husika. Kwaiyo tunagundua kuwa hakuna raia wa Tanzania anaependa kuachana na uraia wake kwa makusudi kabisa ili awe mathalani, Mfaransa ama Mjerumani.
Mara kadhaa, ninewahi kuwasikia Maafisa uhamiaji na wanasheria wakitumia neno "kuukana uraia wa Tanzania" wakijaribu kuelezea dhana ya wanadiaspora wenye asili ya Tanzania waliolazimika kuwa raia wa nchi nyengine, kinachotokea ni kwamba kwa kuwa sheria za uhamiaji na uraia za Tanzania haziruhusu uraia pacha, ndio kusema katika uasili wa sheria hii; raia yoyote wa Tanzania anaechukua uraia wa nchi nyengine sheria hii inamkaana ama kumkataa kuwa si raia wa Tanzania. Naomba nifahamike vizuri sio raia aliukana uraia wake, la hasha ni sheria ndio imemkana mtanzania huyu kwasababu ya yeye kuchukua uraia wa nchi nyengine. Nasema hivi kwasababu ziko nchi ambazo sheria zake zinakubali uraia wa nchi mbili, hivyo unaweza kuwa raia katika nchi hizi sambamba na kubaki na uraia wa nchi yako ya asili. Mathalani kwa sisi watanzania tunheliweza kuwa raia wa Canada ama USA na kuendelea kuwa na uraia wetu wa Tanzania.
Aidha; ningependa kutoa la moyoni hapa, kuna baadhi ya watanzania walioko ndani ya Tanzania, wakiwemo viongozi wa kitaifa, maafisa serikalini kwamfano maafisa uhamiaji na raia wengine wa kawaida wanawatazama watanzani wenzao ambao wanauraia wa nchi nyengine kama wasaliti na watu wasiofawa kupewa haki yoyote wawapo ndani ya nchi yao ya awali, kiukweli kabisa ni dhambi katika mitazamo yote, si ya kiimani wala kibinaadamu au kisheria, kwanini Mtaliano mzungu mweupe umuheshimu lakini mtanzania mwenzeko kama wewe uanze kumletea shida wakati anapojaribu kurudi kwao. Kiukweli kabisa haipendezi na inaudhi kwelikweli ati leo unapita getini kuja kwenu Afisa uhamiaji anahitaji umuoneshe kitambulisho chako cha ukaazi cha huko unakoishi na wakati tayari uneshamuonesha pasi yako ya kusafiria ya huko unakoishi, na tayari imeahawekwa visa ya Tanzania, na upo kihalali kabisa hadi mamalaka zinakuelewa, maafisa uhamiaji muache kuwafanyia karagha na ujinga watanzania wezenu muwapo katika kazi zenu.
Ni hivi, mtanzania ana asili yake na haitaondoka moyoni mwake katu abadani, kinachotokea ni sheria za uraia na uhamiaji za Tanzania kumkana tu kuwa yeye sio raia wa Tanzania, ila atabaki kuwa yeye ni mtanzania, utaifa wake hautang'oka wala kukimbia moyoni mwake katu abadani.
KUHUSU KUREJEA URAIA.
Sheria za uraia na uhamiaji za Tanzania zimeweka utaratibu wa kuruhusu maombi ya uraia kwa wageni, ambao wameamua kuishi na kuomba uraia wa Tanzania, je sheria hizi hazikutoa nafasi kwa wale watanzania wenye asili ya Tanzania ambao waliamua muda fulani kuwa raia wa nchi nyengine kuurudia uraia wao wa awali?.
Nini tunajifunza baada ya kupitishana na kueleweshana utaratibu unaofuatwa kwa nchi ya India na Ethiopia?