Diaspora: Nani yupo Moscow tuonane nipate kampani

Diaspora: Nani yupo Moscow tuonane nipate kampani

herikipaji

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2016
Posts
1,198
Reaction score
1,369
Wasalaam wapendwa!

Heading ya mada inajieleza vizuri hivi majuzi nilisafiri kidogo kuelekea Urusi nikafikia hapa jiji la Moscow sasa ugeni umenizidi huku natafuta hawa ndugu zetu diaspora walioko hapa Moscow tafadhari usomapo hii mada fanya tutafutane sisi ni Watanzania tukiwa foreign land sote ni ndugu.

Mje mnikaribishe na mnipe kampani yenu hapa ukiwa wa kiume ni vizuri na kama wewe ni wa kike ni vizuri pia.

Nimebeba na vijizawadi kidogo kutoka kwetu nyumbani Tanzania hivi ni kwa ajili yenu ndugu.

Karibuni sana.
 
Mbona Wabongo ni wengi sana hapo Moscow? Tafuta msichana wa Kirusi akuelekeze viwanja wanavyoenda mablacks usiku, utawapata wengi tu. Pia ukipita vyuoni utakutana nao wengi sana. Umenikumbusha mbali sana, Niliwahi kuishi Sankt Peterburg!
Shukrani ngoja nimtafute mrembo mmoja wa kirusi hapa anipe ramani haraka iwezekanavyo.
Halafu ubalozi wa Tanzania upo hapahapa Moscow au hakuna?

Saint Petrsburg ulikuja mwaka gani ulikuja kusoma nini?
 
Mbona Wabongo ni wengi sana hapo Moscow? Tafuta msichana wa Kirusi akuelekeze viwanja wanavyoenda mablacks usiku, utawapata wengi tu. Pia ukipita vyuoni utakutana nao wengi sana. Umenikumbusha mbali sana, Niliwahi kuishi Sankt Peterburg!
Wewe ndio yule paka aliyekanyagwa na gari akifanya yake mitaa ya St Petersburg ?
 
Saa izi usimwamini mtuu na hiii sakasaka ya jamiiforum lazima watu tugutuke.
 
Upo mbali sana,mimi nipo hapa mji wa omsk baridi balaa
 
Back
Top Bottom