Diaspora rudini nyumbani

Huyo ndugu yako mmoja. Ha reflect matukio ya watu wote walioko nje.
Mbona wako wanaokuja kuzika na wanarudi nje kuendelea na kazi?
Hapa mtaani kwetu kuna mtu alimtembelea ndugu yake Dar na alimkuta ndugu yake anafanya biashara ya pombe za kienyeji kule Keko na alivyorudi kijijini akatangaza vijana wote waliokimbilia Dar wanauza pombe na kukaa juani kuuza maji Nafikiri hii ni tabia ya watu wa vijijini kama huyu mtoa mada
 
Mtu aache maisha ya fedha na mshahara mkubwa aje kukosa ajira huko na kuishi chini ya dikteta? Hali ya Tz imekuwa mbaya zaidi ya siku zilizopita.
 
Sijawapenda Mkuu but kubeba box ni inclusive zaidi hata walimu wanaweza kuingia humo

Kuna jirani yetu watoto wake wawili wapo germany na USA hawa wana permanent jobs
Ila wanatamani kurudi nyumbani, wanakiri life is so expensive

Mfanyakazi anayelipwa milion moja Tanzania anaweza kuwa na maisha mazuri zaidi kuliko mfanyakazi anayelipwa milion saba in western
 
Kwamba maisha ya watoto wa jirani yako yana relfect diaspora wote? Data za wizara zinaeleza something else bro.
Kwamba mtanzania hana maisha magumu?
Kodi ni kubwa sababu currency ni kubwa. Uchumi mkubwa una demand kubwa ya kodi ili kuuwezesha kubaki kwenye hizo level.
But they have better lives than us.
Huwez sema mtu ana permanent job nzuri tu halaf akabebe maboksi. Hiyo theory yako ni very veru very weak.
 
Ume explain vizuri
 
Kuna jamaa wanafuata itikadi zile za aliye juu mshushe muwe sawa.
Inaitwa roho mbaya. Na hii inatokana na umaskini na dhiki iliyokubuhu.
Humfanya maskini atamani aliefanikiwa aporomoke ili awe level zake. Yaan yeye amekosa njia ya kupanda. Anataka wengine wafilisike kama yeye.
Hapa ndipo unajua umaskini hauleti tu ukosefu wa hela.. bali huvuruga akili, na kupandikiza hali ya kutaman wengine washuke.
 
Kwamba maisha ya watoto wa jirani yako yana relfect diaspora wote?

I didn't mean this! Ila nimekupa mfano tu,simaanishi wanaishi maisha magumu Kwasababu wameajiriwa ila kila wakirudi holiday wanasema life is expensive better stay home kama unauhikika wa kuingiza million kwa mwezi

Western maisha ni mazuri kwa sababu wanapata mahitaji yote muhimu lkn kuna waliochapika pia
 
Kama akili za Watanzania ndo hizi.Ndo maana Afrika kusini wameamua kuchukua Walimu wa Kiswahili Kenya.Tuna vijana wengi Graduate mitaani wanaweza kabisa fundisha Kiswahili Afrika kusini lakini eti Kenya ndo wanachukua kazi eti sisi tunasema maisha magumu nje.
 
Yes wapo. Thats why bado wanakuja . Nyumban hapa is not as if ni pabaya.
Ila wakirud hali ya ajira ikoje? Hali ya huduma zikoje?
Kuna possibility wakaja ku struglle all in the name of kodi ndogo.
 
Kuna kamsemo ka kiswahili . Mtegemea Cha nduguye?.... We ndo mkubwa acha mawazo ya kimasikini kwa tuoffer tudogotudogo ..Kama iPhone na kusomeshewa..... Ukate viuno wewe wengine wakusomeshee what a shame... Ni Bora hiyo misaada ukaielekeza kwenywe mradi wa kukuingizia kipato.
 
Wenye fikira kama hizo za kurudishana nyuma ndio wapo na pale uhamiaji, yaani mtanzania anawekewa vigezo vigumu kupata passport. Inshort wanadiscourage mtu masikini kupata passport ambayo ni halali yake, waache wakenya wazunguke sisi vijana wetu wabanane hapo hapo kitunda,kariakoo,mwenge, mwanjelwa nk .
Mchawi ni sisi wenyewe, nchi nyingi zinazoendelea kwa kasi wanaencourage watu wake kwenda nje kutafuta maisha kihalali ila hapa bongo ni viceversa, watu wapo ofisini kuhakikisha wenzao hawafanikiwi. Hakuna ofisi naichukua kama ofisi ya Uhamiaji Tanzania yaani Migration hasa pale Kurasini.
 
Akili za kimaskini sana hizi. Kama kumenoga si wapeni kazi hao maelfu ya vijana wanahangaika bila kazi?

endeleeni kusifia huku ndugu zenu wengi wanaumia
 

FYI wengi wao wanakuja sana TZ na wanafahamu nini kinaendelea. Vile vile usisahau kwamba wengi wao wamejiendeleza kimasomo hadi hapo walipo na sio waganga njaa. Wakirudi hata nusu tu nchi itabadilika kwa sababu watakuja na mbinu za kuinua maisha yao binafsi na maisha ya Watanzania wengine, wape muda tu, time will tell.
 
Mungu aliumba nchi (dunia) na mbingu. Mipaka ililetwa na wanadamu tu (tena wakoloni). Ni sawa na kusema kila Mtanzania arudi kijijini kwake. Kwamba yule ambaye yuko Dar es Salaam anasaliti kijiji chake. Watu wenye akili finyu ndio hufikiria hivyo. Kwa wenye akili pana dunia yote ni ya Mungu. Na Mungu hubariki huduma yao popote pale. Kama una akili japo kidogo basi umeelewa.
Kinachowauma ni usaliti, walisomeshwa na nchi kwa fedha za walipa kodi halafu wakaona hawawezi kututumikia wananchi.
 
Walishajiona wako paradise, ndio ushamba wenyewe huo. Rudini huku mwishoe yatawakuta ya Floyd
 
Mawazo ya kimasikini kabisa. Kwa mawazo haya, ndio maana mashirika ya kimataifa, wamejaa Wakenya, Waganda, Wanyarwanda.... Watanzania ni wa kutafuta. Elimu ya kweli ni ile inayomwezesha mtu kutawala maisha yake na kuishi popote.
 

Alafu ni roho mbaya
 
Mtoa mada naamini angekuwa na diaspora akaletewa pesa kufanya japo ka mradi naamini atageuka mchwa maana asilimua 90 ya wana diaspora wameshatendwa na ndg ndo maana hakuna wanachofanya nyumbani maana ni michosho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…