Diaspora Watapata Lini hiyo Tanzanite Status?

Diaspora Watapata Lini hiyo Tanzanite Status?

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Tanzania ni nchi pekee katika ukanda huu yenye wivu wa juu sana dhidi ya raia wake kiasi kuwa hairuhusu raia wake wachukue uraia wa nchi nyingine yoyote. Nchi zote zinazoizunguka Tanzania zilishaona mbali kuwa dunia inabadilika haraka na zikawaachia raia wao kuchukua uraia wa nchi nyingine yoyote bila kupoteza uraia wao wa kuzaliwa. Ramani hii hapa inaonyesha jinsi Tanzania ilivyojitenga ikishirikiana na Ethiopia na Eritrea tu. Swala la Eithopia na Elitrea linajulikana lakini hili la Tanzania halijulikani kabisa zaidi ya sera mbovu tu.
1725834983989.png


Kwenye bajeti ya mwaka huu tuliambiwa sasa hivi diaspora wa Tanzania watapewa hadhi maalum japo siyo uraia pacha; hadhi hiyo itaitwa Tanzanite Status. Swali langu ni je hiyo Tanzanite Status nayo ni kweli au bado ni blah blah tu? Je kama ni kweli, itaaanza lin baada ya kupita bungenii au baadaye watakuja viongozi kuibatilisha? Kwa mfano Profesa Kabudi asiyependa uraia pacha pamoja na kukiri kuwa watoto wake walizaliwa ujerumani, je atakwamisha sera hiyo na kupotezea mbali kabisa swala la Tanzanite Status?
 
wenye madaraka hii nchi wanaifanya isiwe beneficial kwa wananchi wa kawaida


hii nchi ngumu sana
 
Back
Top Bottom