Diaspora wengine wamefungiwa ndani -Corona wajulie hali ndugu zako

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Bahati nzuri kazi yangu binafsi naweza kufanya nyumbani na ingawa nipo kwenye mambo ya Afya nafanya kama consultant na kusaidia Hospitali kwenye mikataba ya ununuzi. Kuna Watanzania wengi sana ambao wanafanya kazi za huduma za kiafya hawa wote wapo hatarini sana.

Vifaa hakuna vya kutosha maana kila mtu kakimbilia na kununua. Yaani kuna sehemu hata kwenye store hakuna vitu kama vyakula vya watoto, mayai n.k. Watanzania ambao wapo nchi za EU wapo hatarini lakini na wale wote kwa US waliopo New York, Washington, na miji ya California wapo hatarini sana kwa sasa.

Kama una ndugu yako yupo kwenye unesi au shughuli za kiudumu za Afya muombee na wasiliana naye. Kuna ndugu Tanzania sio wote lakini wenyewe ni wapokeaji tu ni wazuri sana kuomba pesa na kutoa list za matatizo ya pesa ili utume kidogo unachopata. Lakini hawa ndugu ukipata shida kwasababu tu unaishi US, Canada au nchi za EU wanafikiri hauna shida kumbe wengine maisha yao yako hatarini kila siku.

Kuna Watanzania mfano wana biashara za ambulance wanabeba wagojwa kila siku na hata wa Corona halafu message wanazopata ni za kuomba pesa tu. Hivyo mimi nashauri kama una ndugu huu ni wakati wa kumjulia hali maana Corona ya Tanzania sio kama huku.
 
Nchi za ulaya utasikia hakuna Mayai ni kwasababu ya kutafuta kinga

Four vaccines, including those for yellow fever, influenza, measles mumps rubella (MMR), and rabies, contain small amounts of egg protein because they're cultured either in eggs or in chick embryos. 1 This raises a potential concern for people who are allergic to egg protein.
 
ingawa nipo kwenye mambo ya Afya nafanya kama consultant na kusaidia Hospitali kwenye mikataba ya ununuzi.
Hii haikupi hadhi yoyote ya kuyaandika uliyoandika kwenye mada kuhusu hali za waTanzania ambao kazi zao zinahusu utoaji wa huduma za afya.

Kifupi ni kwamba huna ufahamu wowote juu ya utendaji kazi za aina hiyo.

Huu ukonsultant wa mauzo bila ya background yoyote ya mambo ya afya, inatia shaka sana.

Juu ya habari ya hayo mayai, na vaccine zinazotengenezwa humo na 'allergy', navyo ukavitupia kwenye mada ili iweje?
 
Nimesikia ma daktari na manesi kwanza watoto wao wanapata child care mashuleni ingawa shule zimefungwa.

Public transport ina chelewa kwakua madereva wengi wako kwenye self isolation. Ukichukua tax na tax driver akijua kuwa wewe ni daktari au nesi unakwenda kazini hatozi nauli.
 
Hii haikupi hadhi yoyote ya kuyaandika uliyoandika kwenye mada kuhusu hali za waTanzania ambao kazi zao zinahusu utoaji wa huduma za afya.

Kifupi ni kwamba huna ufahamu wowote juu ya utendaji kazi za aina hiyo.

Huu ukonsultant wa mauzo bila ya background yoyote ya mambo ya afya, inatia shaka sana.

Juu ya habari ya hayo mayai, na vaccine zinazotengenezwa humo na 'allergy', navyo ukavitupia kwenye mada ili iweje?

Nafikiri hujanielewa mimi sitoi elimu ya Afya. Hii topic ni ya kujuana hali tu. Nachosema hapo ni kwamba kama una ndugu zako uwasalimie maana inawezekana wanapitia wakati ambao ni mgumu sana kwa sasa. Hii sio topic yangu binafsi au kujipngelea nia ni kujulisha tu
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Bahati nzuri kazi yangu binafsi naweza kufanya nyumbani na ingawa nipo kwenye mambo ya Afya nafanya kama consultant na kusaidia Hospitali kwenye mikataba ya ununuzi. Kuna Watanzania wengi sana ambao wanafanya kazi za huduma za kiafya hawa wote wapo hatarini sana.

Vifaa hakuna vya kutosha maana kila mtu kakimbilia na kununua. Yaani kuna sehemu hata kwenye store hakuna vitu kama vyakula vya watoto, mayai n.k. Watanzania ambao wapo nchi za EU wapo hatarini lakini na wale wote kwa US waliopo New York, Washington, na miji ya California wapo hatarini sana kwa sasa.

Kama una ndugu yako yupo kwenye unesi au shughuli za kiudumu za Afya muombee na wasiliana naye. Kuna ndugu Tanzania sio wote lakini wenyewe ni wapokeaji tu ni wazuri sana kuomba pesa na kutoa list za matatizo ya pesa ili utume kidogo unachopata. Lakini hawa ndugu ukipata shida kwasababu tu unaishi US, Canada au nchi za EU wanafikiri hauna shida kumbe wengine maisha yao yako hatarini kila siku.

Kuna Watanzania mfano wana biashara za ambulance wanabeba wagojwa kila siku na hata wa Corona halafu message wanazopata ni za kuomba pesa tu. Hivyo mimi nashauri kama una ndugu huu ni wakati wa kumjulia hali maana Corona ya Tanzania sio kama huku.
Ndugu yangu ni ujumbe mzuri, mimi naishi hapa Europe miaka 25 sasa kila siku natuma fedha nyumbani kutatua matatizo madogo madogo lakini kwa sasa siwezi sababu kila kitu kimefungwa lakini kila siku napata ujumbe wa kutuma fedha huko, kana kwamba hawajui kinacho endelea hapa, kusaidia ndugu huko Afrika ni jambo la kawaida lakini kwa sasa hapana subirini.
 
Kuna ndugu Tanzania sio wote lakini wenyewe ni wapokeaji tu ni wazuri sana kuomba pesa na kutoa list za matatizo ya pesa ili utume kidogo unachopata. Lakini hawa ndugu ukipata shida kwasababu tu unaishi US, Canada au nchi za EU wanafikiri hauna shida kumbe wengine maisha
[
/QUOTE]

Haya sasa masimango vandugu
 
Haya sasa masimango vandugu

Sio MASIMANGO ni kweli kabisa, kwa watu wasio na exposure wakisikia mtu yuko Ulaya, picha inayokuja kichwani mwao basi jamaa atakuwa anachota pesa kwa beleshi tu. Kumbe, hawajui tu tabu za ulaya
 
Bahati nzuri kazi yangu binafsi naweza kufanya nyumbani na ingawa nipo kwenye mambo ya Afya nafanya kama consultant na kusaidia Hospitali kwenye mikataba ya ununuzi. Kuna Watanzania wengi sana ambao wanafanya kazi za huduma za kiafya hawa wote wapo hatarini sana.

Vifaa hakuna vya kutosha maana kila mtu kakimbilia na kununua. Yaani kuna sehemu hata kwenye store hakuna vitu kama vyakula vya watoto, mayai n.k. Watanzania ambao wapo nchi za EU wapo hatarini lakini na wale wote kwa US waliopo New York, Washington, na miji ya California wapo hatarini sana kwa sasa.

Kama una ndugu yako yupo kwenye unesi au shughuli za kiudumu za Afya muombee na wasiliana naye. Kuna ndugu Tanzania sio wote lakini wenyewe ni wapokeaji tu ni wazuri sana kuomba pesa na kutoa list za matatizo ya pesa ili utume kidogo unachopata. Lakini hawa ndugu ukipata shida kwasababu tu unaishi US, Canada au nchi za EU wanafikiri hauna shida kumbe wengine maisha yao yako hatarini kila siku.

Kuna Watanzania mfano wana biashara za ambulance wanabeba wagojwa kila siku na hata wa Corona halafu message wanazopata ni za kuomba pesa tu. Hivyo mimi nashauri kama una ndugu huu ni wakati wa kumjulia hali maana Corona ya Tanzania sio kama huku.
Kwa hiyo unataka nini hasa? kwanza hayo magonjwa ya wazungu sisi hayatuhusu
 
Sio MASIMANGO ni kweli kabisa, kwa watu wasio na exposure wakisikia mtu yuko Ulaya, picha inayokuja kichwani mwao basi jamaa atakuwa anachota pesa kwa beleshi tu. Kumbe, hawajui tu tabu za ulaya
Hii sio ulaya tu hata hapahapa nchini, hali imebadilika lakini watu wanakomaa kuomba hata ukimwambia sina anajua umemnyima hii ni kasumba yetu sie watanzania na sijui kwanini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom