Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB)
Siku moja mwaka wa 2008 nilipokea email kutoka kwa Prof. Emmanuel Akyeampong kutoka Harvard akaniomba niwe mmoja wa waandishi karibu 500 kutoka kila pembe ya dunia watakaoandika kamusi ya watu mashuhuri Afrika.
Mradi huu ulikuwa unajulikana kama Dictionary of African Biography.
Huu ulikuwa mradi wa Harvard na Oxford University Press New York.
Prof. Akyeampong akaniomba pia niwe mshauri wake kwa majina ya Watanzania ambao mimi naona wamefanya makubwa kwa hiyo wanastahili maisha yao kuandikwa katika hii kamusi.
Prof. Akyeampong akaniomba mimi niandike maisha ya Kleist Sykes lakini yeye alimkusudia Mayor Kleist Sykes.
Mimi hapo hapo nikaanza kazi yangu ya ushauri.
Nikalikata jina la Kleist rafiki na ndugu yangu nikamshauri Prof. Akyeampong kuwa anaestahili kuingia katika DAB ni babu yake, Kleist Sykes Mbuwane (1894 - 1949) na si huyu Kleist mjukuu wa Kleist Sykes Mbuwane, mtoto wa Abdul Sykes.
Prof. Akyeampong alivutiwa sana na kile alichosoma kutoka kwangu kuhusu babu yake Mayor Kleist na kamusi ilipochapwa mwaka wa 2011 maisha ya Kleist Sykes Mbuwane babu yake Mayor Kleist yakawa ndani ya DAB.
DAB ina volume sita na ni maarufu hivi sasa duniani kama kitabu vya rejea kwa watu mashuhuri na mashujaa wa Bara la Afrika.
Lakini wakati naingizwa kwenye radi huu wa DAB nilikuwa nimetoka katika majonzi ya vitabu vyangu viwili kushindwa kukubalika nchini.
Wachapaji wa vitabu hivyo, ''The Torch on Kilimanjaro,'' (Oxford University Press, Nairobi 2007) na ''Uamuzi wa Busara,'' Abantu Publishers, Nairobi 2008) walinihakikishia kuwa kwa maoni yao ni vitabu ambavyo bila shaka yoyote vitatumika mashuleni.
Hili halikutokea na sababu haikuwa kuwa vitabu havikufikia viwango.
NYONGEZA:
Nimeweka hapo juu ''cutting'' ya Sunday News la 20 September, 1968, ''Abdul Sykes was a TANU Pioneer.''
Alipofariki Abdul Sykes magazeti yote ya TANU - The Nationalist na Uhuru hayakumwandika marehemu kama alivyostaili kuandikwa kwa kueleza mchango wake katika TAA hadi TANU, mfadhili wa harakati za uhuru nk.
Mhariri wa magazeti haya alikuwa Benjamin William Mkapa na kilichoandikwa katika magazeti haya ni kuwa Julius Nyerere, Rais wa Tanzania amehudhuria mazishi ya Abdul Sykes.
Hapakuandikwa zaidi ya hayo.
Marafiki wa Abdul Sykes walisikitishwa sana na jambo hili kwani walitegemea magazeti haya yangeandika taazia yenye heshima inayomstahili muasisi wa TANU na mtu aliyempokea Nyerere Dar es Salaam.
Mhariri wa Tanganyika Standard, Mwingereza Brendon Grimshaw yeye ndiye aliyeandika na kuchapa makala hayo hapo juu katika gazeti lake akimnadi Abdul Sykes kuwa ni muasisi wa TANU.