Kukujibu maswali lako labda nianze hivi
Haya mapinduzi yote ya kwenda space yalianza tu baada ya vita ya pili ya Dunia, na ukweli juu ya hiyo ni kuwa, Hitler alikuwa yupo Advanced sana katika modern sciences by that time, Ukiangalia documentary na history mbalimbali za Hitler yeye alishafikia kwenye stage ya kutengeneza Jet engine, computers na vitu vingine vingi japo dunia ya Waamerika na Warusi walikuwa Hawajafikia hiyo stage
Wakati Warusi na Wamarekani na jamaa zake (Waingereza na Wafaransa) wanaingia German, Warusi waliingia upande wa East na wamarekani upande wa West, na walikutana Berlin na hapo ndipo ulipokuwa mpaka wa East na West German (Ukuta wa Berlin), Lakini Warusi ndio walikuwa wa Kwanza kuingia Berlini na walifanikiwa kuingia kwenye ma-Bunker ya Hitler na kuwakuta wanasayansi wengi wa Hitler Pamoja na Modern Equipments ambazo hata kwenyehiyo vita zilikuwa hazijatumika bado na wala wao (Warusi) hawakuwa nazo, Warusi walichukua vitu vingi pamoja na hao wanasayansi, Marekani alikuta mabaki tu na kwa miaka mingi ya mwanzo baada ya vita ya pili ya Dunia Marekani walikuwa wanaangaika kuwatafuta wanasayansi wa Hitler ili waweze kuwatumia kwenye mambo yao ya kisayansi
Warusi waliweza kuwatumia vizuri sana wanasayansi wa Hitler kwenye sector ya Silaha na hii ya Space, Robot, Computer, Jet engines nk, kiwango alichokifikia Mrusi kwenye sayansi hiyo kwa kipindi kile ilikuwa juu sana Zaidi ya Wamarekani na ndio maana hao Warusi ndio wanaonekana kama baba wa Space
Kwa kujibu maswali yako
1) Sio kwamba hiyo Technologia ya kwenda Mwezini na kurudi kwa sasa kuwa hipo, bali hata miaka ile ya 50s na 60s hiyo technologia ilikuwepo
Mwaka 1957 Warusi ndio walikuwa watu wa kwanza kuweka satellite kwenye orbit
1957 walifanikiwa kupeleka kiumbe hai (Mbwa-Laika) kwenye space
1961 chombo cha kwanza chenye mtu (manned spacecraft) kwenda Space na kufanya Mzunguko kwenye orbit (hapo alikuwa ni baba wa Space Yuri Gagarin alikufa 1968 kwenye crash ya MiG-15)
Mwaka 1965 mwana mama Valentina (mwanamke wa kwanza space), na mwaka huo huo Leonov alikuwa ni mtu wa kwanza kutembea space, pamoja na hayo yote Warusi walishapeleka Chombo mwezini na Maroboti na walikuja na evidence za 326g za mawe ya mwezini
Baada ya Wamarekani kuona hayo mafanikio makubwa ya Warusi na Wajamaa wote Duniani (Kumbuka dunia ilikuwa kwenye vita baridi), kwao ilikuwa haina budi kutengeneza kitu kikubwa cha kuweza kuiangusha Urusi kwenye hiyo record na ndio kisa cha kutengeneza hiyo movie ya Apollo 11 ndani ya jangwa la Nevada kwamba wamefika mwezini na kupata kilo 382 za mawe ya mwezini zaidi gramu 326 za Warusi (WaAustralia walikuwa na evidence nyingi mno za Apollo 11 kwani by that time wao walikuwa na uwezo wa kupata picha na sauti safi kutoka Jangwani Nevada ilipokuwa inafanyika hiyo movie kwani wamarekani waliirusha live, -NASA wamejitahidi kwa miaka mingi kuzitafuta kopi ili waziharibu- kwani kuna kipande cha picha za mwezini kilikuwa na Kopo la Cokacola)
Kwa hiyo uwezo wa kwenda na kurudi upo ila Warusi walishafanya research kubwa sana ya space na conclusion ilikuwa ni vigumu sana kwa kiumbe kuweza kufika na kutembea juu ya mwezi miongoni mwa hiso sababu ni Radiations/Cosmetic rays, Solar flares na Solar Winds
2) Trip ya Kwenda Mars kwa (Unmanned spacecraft) inawezekana kabisa kuwa ya ukweli, japokuwa Wamarekani ndio waliotuma hicho kitu (Rover) Mars lakini Dunia nzima hasa ile yenye technologia (Russia, China na hata Japan) pia walifanikiwa kupata picha za huko through that Robot
Lakini Tatizo la kupeleka mtu kule (Mars) linabaki palepale (Radiations/Cosmetic rays, Solar flares na Solar Winds) na Tatizo lingine linalijitokeza ni Uzito wa chombo kitachoenda na mtu Mars (Consumables na fuel), niliwahi ona Documentary iliyotoka NASA to Puplic walikuwa wanazungumzia uwezekano wa kutengeza chombo ambacho kitakuwa na mechanism ya kuibadilisha hewa ya huko (N, H, C) pamoja na O2 ili kuwa Fuel itakayotumiwa na Hicho chombo wakati wa kurdi Duniani, yaani kitaenda na mafuta kidogo tu ya kufika huko na mafuta ya kurudi yatengenezwa huko huko
ni story nzuri anyway