Diddy kubaki jela hadi 2025, akosa dhamana tena

Diddy kubaki jela hadi 2025, akosa dhamana tena

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Mahakama ya New York, Marekani imekataa ombi la Msanii, Sean “Diddy” Combs kutaka kuachiliwa kwa dhamana na kuishi katika nyumba binafsi (Appartment) wakati akisubiri kesi inayomkabili ya mashtaka ya usafirishaji wa Binadamu kwa ajili ya unyanyasaji wa kingono kuanza kusikilizwa mwakani 2025.

Jaji anayesimamia kesi hiyo aitwaye Arun Subramanian amesema hakuna masharti yanayoweza kuhakikisha usalama wa Jamii kutokana na tabia za Diddy Combs alizofanya katika kesi zinazomkabili huku Msanii huyo akihofiwa kuwa endapo atapewa dhamana atawatisha Mashahidi.

Mawakili wa Combs walitaka Mteja wao aachiliwe kwa dhamana ya dola milioni 50 (zaidi ya shilingi bilioni 125 za Kitanzania) na kugharamia ulinzi pamoja na kuishi katika nyumba binafsi (Appartment) lakini ombi hilo limetupiliwa mbali na Mahakama, Msanii huyo akiendelea kusalia gerezani.

Combs alikamatwa mwezi Septemba mwaka huu na amekana mashtaka yote yanayomkabili, kwa sasa anazuiliwa katika gereza la Metropolitan Detention Center, Brooklyn huko New York, Serikali inasisitiza kuwa kuachiliwa kwake kunaweza kuhatarisha usalama wa Mashahidi na Jamii.

“Tutapigania kesi hii kwa kila kitu tulicho nacho, kama anavyofanya yeye, na mwishowe, atadhihirika kuwa hana hatia” —— Wakili wa Diddy Combs, Mac Agnifilo amesema, Kesi ya Msanii huyo imepangwa kuanza kusikilizwa rasmi mwezi Mei mwaka 2025.
#Mill
1732943848397.jpg
ardAyoENT
 
Back
Top Bottom