Diego Costa ahukumiwa miezi 6 kwa kosa la kukwepa kodi katika uhamisho wake mwaka 2014

Diego Costa ahukumiwa miezi 6 kwa kosa la kukwepa kodi katika uhamisho wake mwaka 2014

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
external-content.duckduckgo.com.jpg

MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Diego Costa amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela, amacho hatakitumikia na faini ya jumla ya Pauni 482,000 baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa kodi zaidi ya Pauni 900,000 mwaka 2014.

Kwa mujibu wa mahakama, mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 31 hakulipa kodi baada ya uhamisho wake Pauni Milioni 4.4 kwenda Chelsea mwaka 2014 na malipo ya haki za pcha zake, zaidi ya Pauni 900,000.

Sheria ya Hispania inatoa fursa kwa wanaohukumiwa kifungo cha chini ya miaka miwili kulipa faini badala ya kuwekwa gerezani.

Na Costa alikubali kulipa faini ya Pauni 32,000 baada ya kulipa Pauni 450,000 ili kukwepa kuwekwa jela.

Mamlaka ya Kodi Hispania imekuwa mwiba wanasoka nyoata hivi karibuni, ikiwachukulia hatua hadi akina Lionel Messi na Cristiano Ronaldo na kocha wa zamani wa Real Madrid, Jose Mourinho na hakuna kati yao aliyetumikia kifungo baada ya wote kulipa faini.
 
Dawa kukata uraia wa nchi nyingije kama hutaki kuchangia maendeleo ya nchi yako kwa mujibu wa sheria mlizojiwekea ninyi wenyewe.
 
Ingekuwa ni Tanzania ,chadema wangepinga vibaya sana na kusema ameonewa tu kwa kuwa ni mkereketwa wa upinzani
 
Back
Top Bottom