Diego Maradona atangaza nia ya kutaka kumrithi Blatter

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
402
Reaction score
252

NGULI wa soka wa Argentina, Diego Maradona ameamua kugombea nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kuchukua nafasi ya rais wa sasa Sepp Blatter.

Kwa mujibu wa mwandishi na mtunzi Victor Hugo Morales amedai kuwa maradona alimwambia nia yake hiyo wakati alipompigia simu kutaka kujua kuhusu hali ya baba yake aliyekuwa mgonjwa jana.

Morales amesema Maradona alimwambia kuwa anataka kugombea nafasi hiyo na kumruhusu kutangaza taarifa hizo. Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro mapema mwezi huu alimpigia chapuo Maradona kuwa rais ajaye wa FIFA.

Maradona mwenye umri wa miaka 54 amekuwa akimpiga Blatter kea kipindi kirefu na mwezi uliopita alidai kuwa amefurahi kuibuka kwa sakata la rushwa ambalo lilipelekea rais huyo kutangaza kuachia ngazi.

Wengine waliojitokeza kuitaka nafasi hiyo ni pamoja na nguli wa soka wa Brazil, Zico pamoja na mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Liberia Musa Bility.

Chanzo: Beki3


 
Huyo mtambo hawezi kupata kura hata 10.

Huyu naye ni kigeugeu tu.. mana Blater alipotangaza kuachia ngazi, akasema anatarajia kua vice wa Bin Ali.. sasa kaona huo u_vice haumtoshi anataka upresidaa.. hata hizo kura 10 hatopata, ataishia 1 toka argentina.
 
Maradona marufuku kuingia uingereza waingereza wanamchukia zaid ya shetan blatter resign ilikua pull up by us and uk thus y fbi wanataka kum sue blatter alafu wasiempenda awe rais hakunaga io
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…