Difference between Police and Army

Srebrina

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2012
Posts
958
Reaction score
426
Habari za kazi ndugu na jamaa, nina kitu naomba tusaidiane uelewa maana nimetafuta majibu mpaka sasa nashindwa kuelewa utofauti, nauliza ivi kuna utofauti gani kati ya police na army?

Maana nikisikia jeshi la polisi najua polisi ni jeshi mara naambiwa polisi sio jeshi yaani nashindwa hata kuelewa nani ni nani
 
Tafsiri ya jeshi ni muunganiko wa viumbe fulani ili kukabiliana na kitu fulani we hukusikiaga kule china waliandaa jeshi la bata kukabiliana na nzige..😅
 
Polisi ni huduma ya kiusalama (inapaswa kuwa police department) na katika nchi za walioendelea ndivyo ilivyo.

Jeshi ni chombo maalum kwa ulinzi wa mipaka ya nchi kwa maana ya kupambana na maadui wanaotishia amani au kuvamia nchi.
Kwa Tanzania jeshi linatakiwa kuwa moja Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), hawa wengine wanapaswa kuwa idara za kiusalama tu.

Sasa polisi inakuwa jeshi inapambana na nani?
Polisi kuwa jeshi inaleta ukakasi sana
 
Kwa mujibu wa Katiba yetu yote ni Majeshi tofauti ni majukumu.
Kwaiyo mkuu terms zao za ufanyaji kazi ndio zinatofautiana, na hakuna kwamba nani yuko juu ya nani? Au kwamba polisi wako chini ya wanajeshi kwakuwa hawalindi nchi na mipaka Bali usalama Wa RAIA? Na vipi mfano najua ikitokea Raisi kaenda kwenye maonesho mfano ya Uhuru kunakuwa na police na wanajeshi vipi kuhusu heshima maana mi najua kitu muhimu sana kwenye izi organ ni heshima vipi kuhusu coplo Wa jeshi akikutana na afisa Wa police?
 
Mkuu unaposema kupambana unamaanisha nn maana hata police wanapambana na wahalifu na majangiri waliopo ndani hata kama wawe wametoka nje ya nnchi
 
Mkuu unaposema kupambana unamaanisha nn maana hata police wanapambana na wahalifu na majangiri waliopo ndani hata kama wawe wametoka nje ya nnchi
Hao ni hawalifu wa kawaida tu ambao hukamatwa na polisi, wavamizi wa nchi ni jukumu la JWTZ hata kama watashirikiana na polisi lakini bado itakua ni mualiko tu.
 
Jeshi la wananchi-linapambana na wananchi
jeshi la polisi -linapambana na polisi
jeshi la magereza-linapambana na magereza
jeshi la konde boy-linapambana na wasafi
jeshi la mtu mmoja-linapambana na fid q


nakuja kuendeleea....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…