Differential lock system

Codeblack

Member
Joined
Dec 23, 2012
Posts
95
Reaction score
45
Kwa mwenye uelewa mpana kuhusu hii system na ufanyaji kazi wake naonba anieleweshe..
 

Attachments

  • 1475174836900.jpg
    12.3 KB · Views: 144
Nikujibu kwa maelezo marefu. Jaribu kufikiria gari ikitembea huku imekata kona itatengeneza duara 2. Tairi iliyo nje itatengeneza duara kubwa ya ndani duara dogo (unaweza ukachora kuthibitisha) na ukipima umbali tairi la nje linakuwa limetembea umbali mrefu kuliko la ndani sasa kazi mojawapo ya difu ni kugawa nguvu (speed) tofauti kwenye kona coz tairi la kushoto na kulia yakipata nguvu sawa ufanisi wa mfumo wa usukani unakuwa hovyo (gari ikiwa speed kali haitakata kona japo tairi za mbele zitakuwa zimekata). gari inapokwama matopeni ni matokeo ya difu kupeleka nguvu zote kwenye tairi ambalo halijakanya chini so litazunguka lkn haliwezi kukwamua gari (nadhani umeshuhudia gari ikikwama tairi huzunguka moja) SASA kazi DIFF LOCK botton ni kulazimisha difu kugawa nguvu sawa kwa tairi zote mbili ili kukwamua gari (TAHADHARI MARA UKISHAKWAMUA GARI HAKIKISHA UNAZIMA DIFF LOCK KUPATA UFANISI WA USUKANI MARA ZOTE UKIWASHA DIFFLOCK TAA NYEKUNDU HUWAKA KWENYE DASHBOARD KUKUTAHADHARISHA)
 
Shukrani mkuu kwa maelezo yako..Je ni sawa na tunavyosema 4wheel drive?. Maana nimezoea kusikia mfano gari ikikwama kwenye matope au mchanga unaambiwa tumia 4 wheel.
 
Shukrani mkuu kwa maelezo yako..Je ni sawa na tunavyosema 4wheel drive?. Maana nimezoea kusikia mfano gari ikikwama kwenye matope au mchanga unaambiwa tumia 4 wheel.
DIFFLOCK na 4WD ni vitu tofauti japo vyote vinasaidia kukwamua gari lililokwama. 4WD ni gari ambalo engine inapeleka nguvu tairi zote (mbele na nyuma) mfano landrover, landcruiser nk. Japo gari kuwa na 4WD hakuzuii gari kukwama endapo tairi 2 (1 mbele 1 nyuma) hazitakanyaga ardhi ndio maana kuna gari zina difflock na 4wd so ukikwama unaweka 4wd ikishindwa unaweka difflock ikishindwa KAPIGE RAMLI
 
Mkuu.. Sina cha kuongeza.. Nadhani umemaliza kila kitu...
 
Asee shukrani mkuu nimekupata vyema kabisa
 
Upo fit
 
Asee shukrani mkuu nimekupata vyema kabisa
Chukua na hii kuhusu uhusiano wa gari, tairi na ardhi. Kwa Tanzania tuna magari mengi specification zifuatazo. 4×2, 4×4, 6×2, 6×4, 6×6. Tarakimu ya kwanza ni idadi ya hub(tyre location) na tarakimu ya pili ni idadi ya hub zinazosukuma gari. Mfano 4×2 ni kama Canter ina hub 4 lkn zinazosukuma gari ni 2 za nyuma. 4×4 ni kama l/cruiser ina hub 4 na zote zinasukuma gari. Nadhani nimesomeka
 
Dah!nakuelewa mtaalam!
 
Dah!kuna kitu kimenisumbua muda mrefu sana,kuna gari nimeshawah kuendesha ni front wheel,asa kuna cku nilikwama,tairi moja ya mbele ilikuwa imekanyaga ardhi na nyingine inazunguka ipo juu,asa nikajiuliza kwa nn hii tairi ilioshika ardhi isisukume kutoa gari?!kwa kweli cjapata majibu mpk leo,naomba unieleweshe hapo
 
Diff ni kama mizani (beam balance) ikitokea tairi moja lina mzigo lingine liko huru nguvu yote itaenda kule kusiko na mzigo hii imewekwa kusaidia gari kukata kona (rejea maelezo hapo juu) inapotokea gari imekwama ni hasara ya kimfumo so dawa ni kuvuruga mfumo huo kwa muda (difflock) au kulidhibit tairi linalozunguka (matrekta yana brake pedal mbili kwa matairi ya nyuma so ikitokea hali iliyokukuta unakanyaga brake ya tairi linalozunguka ili lililoganda lianze kufanya kazi)
 
labda kuongezea unapoweka diff lock ni sawa na four wheel maana hapo ni tairi zote zinakwenda kwa mzunguko uliosawa. kwa mfano rav4 ziko za 2 wheel na 4 wheel. unapokuwa na ya 4 wheel kama haina lock diff ikiua shaft ni ngumu kutembea ila kama ina lock diff unaweza kutoa shaft husika na ukaendelea na safari
 
We jamaa noma!
Sasa humo ndani ya Deff mbona nahisi kama gears zitakuwa zinasuguana sana? Au nini kinahamisha hizo gears /joints ndani ya deff?
 
Ni vigumu kutoa maelezo mpaka ikaeleweka. Difu lina parts zifuatazo: pinion, crownwheel, planet gear, sun gear & drive shaft (axle) sasa meno (gears) ndio yanayohamisha mwendo kati ya pinion>crownwheel & planetgear>sungear>axle, hakuna gear zinazounganisha crownwheel>planetgear ufundi uliotumika kusafirisha mwendo ndio unalifanya difu ligawe speed tofauti(inaelezeka vizuri practically) so difflock ni hali ya kuzifanya axle zipate mwendo kutoka crownwheel bila kupitia planetgear
 
Umejitahidi kuelezea ila sasa umepotosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…