The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,017
- 19,506
Habari wakuu.
Hii biashara ya kutangaza bidhaa zako kwenye mitandao naona bado haijaeleweka vizuri hapa Tanzania.
Wafanya biashara wengi bado wana uswahili mwingi sana. Mtu anatangaza biashara yake mtandaoni hasemi iko wapi, haweki bei na wala hatoi maelezo ya kueleweka.
Mimi ni mpenzi wa kununua bidhaa mitandaoni ila kwa kweli wafanya biashara wetu wengi bado hii fursa hawajaielewa.
Nenda kupatana, unakutana na bidhaa nzuri lakini muuzaji hajaweka bei, hasemi anapatikana wapi na wala hajaweka maelezo ya kutosha kuhusu bidhaa zake, hivyo hivyo zoom Tanzania. Yani anataka umpigie sim ndio umuulize bei ya bidhaa yake muanze kujadiliana.
Wengine wanafanya biashara kupitia social media kama instagram, unakuta mtu kaweka au anatangaza bidhaa au huduma yake cha ajabu account yake kaiweka private, yani hadi umfollow ndio uone anachoiuza, hovyo kabisa.
Online stores nyingine kama jumia, ebay nk wao wanaweka kila kitu ushindwe mwenyewe, watanzania lazima tubadilike, hii mambo ya kufanya biashara kwa mazoea hatuendi popote.
Ahsante.