Kama unataka kusaidiwa toa maelezo yanayojitosheleza, kwa mfano, wewe unataka kusoma fani gani? kwa sababu muda wa masomo haulingani unategeana na aina ya program unayotaka kusoma. Kwa mfano udaktari wa binadamu/wanyama ni miaka 5-7, engineering ni miaka 4 n.k. Ila kwa mfumo wa elimu wa China muda wa chini kabisa kusoma degree ya kwanza ni miaka minne, hii ni kawaida na siyo jambo geni. Hata hapo Tanzania kuna program za shahada ya kwanza za miaka 4 nyingi tu.
Na kwa china kama hujui lugha, kuna mwaka 1-2 wa kujifunza lugha. Labda kama unataka kusoma Hong Kong ambako wanatumia kiingereza vyuo vikuu.
So, what is your problem.