DILI LA WAKENYA hapa NZEGA!mikono ya swetaaa

Ubungoubungo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2008
Posts
2,502
Reaction score
741
JAMANI, ni ajabu nimewakuta wakenya hapa nzega Tabora, wanafanya kampeni ya kutahiri wanaume, hata watu wazima wanapanga foleni wanaenda kutahiriwa ati kwa kufanya hivyo kunapunguza uwezekano wa kupata ngoma. nilijiuliza kuwa hivi watu wa tabora na waasukuma wanaacha mikono ya sweta?, pia, sisi wabongo tumeshindwa kuhamasisha hadi wakenya waaambie wazungu kuwa sisi watz tuna tatizo hilo wakapata pesa na kuja kuzila huku nzega kwa mgongo huo?

cha muhimu pia, JE? NI KWELI KWAMBA MTU ALIYETAHIRIWA ANAWEZA KUFANYA MAPENZI NA MWENYE NGOMA alafu asiathirike? hivi inaingia kichwani kweli jamani?, kama wanasema friction, of which extent ndo inasababisha ngoma, si nasikia hata yale majimaji tu ya ukeni yanakuwa na virusi, sasa yale majimaji ya ukeni yakiingia kwenye mfereji wa urethra si ngoma iko palepale? what is your understanding about this? YAANI WAKENYA WAMEKUJA KUTUTAHIRI SISI WABONGO,WAKATI KULE KWAO WAJALUO kina odinga hawatahiri, kuna kipindi odinga lifanya kampani hiyo kwa wajaluo wenzie.
 
Wewe umetahiriwa??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Chezea Wakenya wewe.... Hawa jamaa wanatushinda kila kitu, japo ni weusi wenzetu. Wameona Watz tumelala wakawahi mkwanja wa mashirika ya Wazungu. Matatizo yetu ni dili lakini hatujitambui. Hii EAC hatuiweziiiii
 
Chezea Wakenya wewe.... Hawa jamaa wanatushinda kila kitu, japo ni weusi wenzetu. Wameona Watz tumelala wakawahi mkwanja wa mashirika ya Wazungu. Matatizo yetu ni dili lakini hatujitambui. Hii EAC hatuiweziiiii
wameacha magovi ya kwao kule kwa wajaluo, wakachukua mkwanja wakaja kukata yale ya watz....changamkia tenda hiyo....
 
Sioni taabu kama hawajavunja sheria!..Watz tumezidi kwa kulialia!! angekuwa mzungu ndio kamleta mzungu mwenzie usingesema!..
 

Isipo tahiriwa basi huna chako mijini kama Dar!
 
Umesema Wakenya wanafanya hii campaign ya kutahiri Nzega? Wanakibali cha nani kufanya shughuli hii?
 

Rudi tena utueleze unaposema wakenya maana yake nini? Je ni kikundi cha raia wa Kenya (madaktari, ma Nurse nk), au ni taasisi/NGO au unamaanisha nini? Kwa uzoefu wangu, NGOs zinazofanya shughuli hii zimesajiliwa Tanzania, na wafanyakazi wake majority ni Watanzania, isipokuwa wakati wa kampeni za uhamasishaji inawezekana wanatumia kampuni za wakenya (na katika hili, iko wazi wenzetu wamepiga hatua katika shughuli za social marketing, na kampeni nyingine)

Ninavyofahamu, male circumcision /tohara ya wanaume imethibitishwa katika tafiti Ulaya, Afrika na kwingineko kuwa inazuia yule aliyetahiriwa kupata virusi vya UKIMWI hadi kwa asilimia 60. Viashiri vingine ambavyo viko wazi (na hasa vilivyochochoea kufanyika tafiti hizi) ni kuwa, jamii ambazo hazitahiri zimeonekana kuwa na maambukizi makubwa zaidi ya VVU kuliko wanaotahiri hata pale watu wa jamii hizi wanapoishi jirani sana. Miji ya Kisumu na Jirani zake, Nchi za West Africa (Muslim vs non Muslim) na hapa kwetu Kanda ya ziwa, shinyanga, Mwanza, vs mikoa ya jirani. Kwa hiyyo kuhusu ukweli juu ya intervention hii, halina ubishi.

Hilo la wakenya toa ufafanuzi.
 
nafikiri kwaajili ya usafi, ni muhimu kutahiri, hata kwenye bible kutahiri kupo na kutotahiri kuko discouraged...sijaelewa unaposema kanda ya ziwa, una maana kanda ya ziwa hawatahiri? wasukuma hawatahiri?, ninuavyo labda baadhi ya wahaya, na baadhi ya watu wa mara, pamoja na kwamba sehemu kubwa ya mara wanatahiri hadi wanawake....shinyanga na mwanza hawatahir? never knew this before.,
 
Ivi mnajua madhara ya kampeni kama izo ni kuwa hao watu baada ya kutailiwa ndo wataanza kupiga kila kona maana kuna watu wamekuwa misunderstood!
TEgemea mlipuko wa ukimwi maeneo hayo after sometimes
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…