Dini imekuja kutugawa au ni sisi ndiyo tumeshindwa kuielewa?

Aelknes

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
246
Reaction score
603
Nikiwa kwenye harakati za utafutaji nikakutana na fursa nikaona niruke nayo maana nakidhi vigezo vyote,Cha ajabu nikaja kukataliwa kisa sio muumini wa DINI fulani...

Nimekua nikishuhudia watu wakitengana,wapenzi wakishindwa kuoana,watu kifanyiana chuki za wazi wazi kisa tu wako na imani tofauti

Imekua kawaida watu kufanya maovu na kujificha kwenye kivuli cha kujifanya mtu wa dini sana

Ni kawaida pia watu wa dini kujitenga kwa kujiona wao ni wa tofauti na watu wengine

Ni kwamba DINI ndo inayotugawa au ni sisi ndo tumeshindwa kuielewa?
 
Sisi ndio tumeshindwa kuielewa. Tena dini usipoielewa vizuri inaweza kukuuwa kabisa na kuharibu maisha yako yote. Kwa bahati mbaya sana wanadamu wamevurugwa sana na dini na pia dini zimetumika kuwapotosha watu na kuwafanya wawe mbali zaidi na Mungu! Kuwa mwangalifu sana na yale unayoyaamini.
 
Dini ni chombo tu, inategemea na mtumiaji.

Mfano ni wakati waingereza walitengeneza bibilia inaitwa 'Select Parts of the Holy Bible: For the Use of the Negro Slaves' kwa sasa 'The Slave Bible' mwaka 1807 kwa ajili ya kuwazuga waafrika.

Visa vingi vinavyohusu kupambania haki kama kisa cha Musa viliondolewa kwenye bibilia hiyo ili waafrika wasipate hayo mawazo.

Mbaya hapo ni bibilia ama ni mzungu?
 
Nikiwa kwenye harakati za utafutaji nikakutana na fursa nikaona niruke nayo maana nakidhi vigezo vyote,Cha ajabu nikaja kukataliwa kisa sio muumini wa DINI fulani...

Nimekua nikishuhudia watu wakitengana,wapenzi wakishindwa kuoana,watu kifanyiana chuki za wazi wazi kisa tu wako na imani tofauti

Imekua kawaida watu kufanya maovu na kujificha kwenye kivuli cha kujifanya mtu wa dini sana

Ni kawaida pia watu wa dini kujitenga kwa kujiona wao ni wa tofauti na watu wengine

Ni kwamba DINI ndo inayotugawa au ni sisi ndo tumeshindwa kuielewa?
Ubinafsi ndiyo tatizo
 
Dini zimetengenezwa ili kumpumbaza mwanadamu na kuendelea kumtawala kupitia imani za hizo dini
 
Dini hatujaielewa tu, tatizo limeanzia hapo, Yesu anasema wapendeni wanaowaudhi lakini sisi tunawapenda wanaotupendeza wasiotupendeza tunawaweka kando, Dini zimetufanya tuone wengine hawafai ila sisi tunafaa, hapo tunakosa unyenyekevu, kuna ndugu mmoja amebidili jina analotumia tumia nyumbani na kazini yako tofauti, Nyumbani anaitwa Fadhili, ila kazini anaitwa Sharif
 
Nikiwa kwenye harakati za utafutaji nikakutana na fursa nikaona niruke nayo maana nakidhi vigezo vyote,Cha ajabu nikaja kukataliwa kisa sio muumini wa DINI fulani...

Nimekua nikishuhudia watu wakitengana,wapenzi wakishindwa kuoana,watu kifanyiana chuki za wazi wazi kisa tu wako na imani tofauti

Imekua kawaida watu kufanya maovu na kujificha kwenye kivuli cha kujifanya mtu wa dini sana

Ni kawaida pia watu wa dini kujitenga kwa kujiona wao ni wa tofauti na watu wengine

Ni kwamba DINI ndo inayotugawa au ni sisi ndo tumeshindwa kuielewa?
Sure mkuu kuna wengine hata harakati za uhuru wanasema sisi dini ndio tulipambana..
Wakati hao wazee kipindi hicho hawakuwa na muktadha ni utanganyika ndio uliwasukuma.
 
Kwa tafsiri yako binafsi Dini ni nini ?; Na je kuna Dini inayosema categorically kwamba wale ni wao na sisi ni sisi ? Na kama ndivyo na hio Dini ipo basi naweza kusema haifai....
naijua ila sitaitaja maana wale waumini huwa wana hasira za haraka
 
Back
Top Bottom