Sauti haki
New Member
- Oct 28, 2020
- 3
- 0
1. Yapo mambo hutokea kwa maombi na mengine hutokea kwa kusaidiana halafu maombi yakafuata. Viongozi wengi wa dini hujua la kuombea na la kuchangia ila huchagua kuombea tu hata vinavyohitaji kuchangia.
2. Kadri dini zinavyofundisha kumpenda Mungu, zifundishe pia wanadamu kupendana.
3. Kwa kadri viongozi wa dini wanapohimiza matoleo, nao pia wapende kutoa ili kusaidia wenye uhitaji ndani ya dini zao. Sio kujilimbikizia mali na utajiri huku waumini wakitaabika kwa shida.
4. Umoja na mshikamano visiishie ndani ya nyumba za ibada halafu wakitoka ibadani hata lifti hawapeani japo wanaenda njia moja. Umoja uwe wa kweli.
5. Waumini wafundishwe kujiwekea hazina mbinguni na kujijenga kiuchumi duniani. Kabla ya kufika mbinguni, kuna maisha wanaishi duniani. Wasiache kuishi vizuri duniani kwa matarajio ya kuja kuishi vizuri mbinguni. Wajifunze kupitia kwa viongozi wao wa dini, hawaishi maisha duni na kimasikini duniani.
6. Dini na wenye dini watenge asilimia 40 ya mapato yao kurudisha faraja na furaha kwa wenye uhitaji, sio wao kukusanya tu pasipo kutoa. Jamii ushuhudie upendo wa Mungu kupitia matendo ya walioshika dini na kumuabudu Mungu.
7. Viongozi wa dini wamepewa mamlaka ya kuongoza imani za watu. Isiwe fimbo ya kuharibu amani, umoja na mshikamano wa taifa kwa kuhadaa wanaowaamini kudharau mamlaka ya serikali.
8. Miradi ya kijamii inayomilikiwa na dini kama vile shule, vyuo na hospitali iwe ni miradi itakayonufaisha jamii na hasa waumini kwa kutoa huduma kwa gharama ya chini na bure kwa yatima, wazee, walemavu na wajane.
Nahifadhi mawazo yangu kuhusu dini katika jukwaa hili, yakisomwa yajenge fikra za wenye dini.