Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Tulikuwa na dili za asili kila pahala ulimwenguni.. Kwenye baadhi ya maeneo mpaka leo zipo na zinaheshimika sana!
Dini hizi ni dini zenye imani juu ya miungu.. Zisizoamini katika Mungu mmoja
Binadamu huwa ni mwepesi kuchoshwa na kitu kilekile kwa wakati wote.
Zikaingia dini zenye kuamini katika Mungu mmoja. Pamoja na tofauti zao kubwa na ndogo lakini bado imani yao ni kwa Mungu mmoja mweza wa yote.. Hata mimi ni mmojawapo mwenye imani hiyo tangu kuzaliwa mpaka sasa
Dini hizi zikaenezwa ulimwenguni kote lakini bado zikishindwa kupenya kwenye baadhi ya maene
Kule ambako zilifanikiwa kupenya watu wengi waliachana na dini zao za asili na kupokea hizi imani mpya
Kwa karne nyingi mambo yameendelea kuwa hivyo lakini taratibu watu wameanza kuzichoka hizi dini zenye imani juu ya Mungu mmoja.. Walimwengu wanataka kitu cha ladha tofauti
Ziliibuka dini zenye imani juu ya shetani lakini uungwaji mkono sio mkubwa sana kwakuwa dini za asili zenye kuabudu miungu na dini mpya zenye kuabudu Mmoja zote kwa pamoja zinamchukulia shetani kama kumbe mbaya
Wao wanachotaka ni imani itakayoleta uwiano kati ya Mungu na miungu. Yani mtu aamini katika Mungu mmoja lakini wakati huohuo awe na imani nyingine ya miungu kama backup
Kwa wale waliowahi kuliona hili ombwe la kiimani waliweza kuchota mamilion ya watu kupitia dini za matukio miujiza na kwa sehemu kubwa ushirikina na mazingaombwe
Ndio hizi dini za watu binafsi zinazoitwa makanisa na vituo vya huduma za manabii ambao wanatembea Mulemule kwenye maandiko ya misahafu lakini matendo yao na mengineyo ni akisi ya dini za asili.
Hawa ni wa mpito tu hata hivyo kuelekea dini moja kuu ulimwenguni kote ambayo ndio itakuja kutawala ulimwengu