Dini mpya yaibuka Tanzania, Kumbukizi miaka 5 iliyopita mwana JF Likud aliwahi sema Genz hawana dini

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Posts
25,050
Reaction score
45,202
Amani iwe nanyi watumishi wa MUNGU katika KRISTO YESU

Hii naichukulia kama kumbukumbu maishani mwangu kwamba usiepende kukaa unapinga kila jambo

Mwana JamiiForums Likud miaka takribani saba iliyopita aliwahi sema humu jukwaan kuwa watoto wa mwaka 2000 hawana dini kipindi hicho jina la Genz likiwa halijashika kasi, mimi binafsi nilimpinga sana

Lakin kuanzia mwaka juzi jambo hili nilianza kulizibitisha mwenyewe kwa macho yangu

Kwanza ikifika saa saba mchana kwa sisi tunaofanyia mishe posta kila mtu huwa anaenda kwenye ibada lakin huwezi muona Genz kaenda kanisani au msikitin saa saba hilo sahau kabisa

Pili wakikuona unapenda sana swala wanabaki wanakushangaa sana wanakuona kama mtu uliyepitwa na wakati

Kikubwa zaid sasa wamekuja na dini yao mpya inaitwa krislam

Hiyo dini hakika inachanganya

Genz mumenishinda tabia

Tukutane D9

LONDON BOY
 
Kwakweli kukuta kijan swala tano unajiuliza huyu kapatwa na nini unamshangaa adi unamuuliza jombi vipi kwani shida nini hhaa mi siku nikasema niende church wana wakashangaa sanaa aaah ahh kanisa limeingiliwa leo mwingine akanambia una lolote umeenda kufuata wachumba tu
 
Nilishangaa kuona sheikh fulani na madevu yake linaimba mapambio na tenzi katika msiba wa bibi yake asiyekuwa muislam, tena lenyewe ndilo lilikuwa linaongoza kuimba nyimbo za maombolezo
 
Nilishangaa kuona sheikh fulani na madevu yake linaimba mapambio na tenzi katika msiba wa bibi yake asiyekuwa muislam, tena lenyewe ndilo lilikuwa linaongoza kuimba nyimbo za maombolezo
umeeleza vizuri tatizo umemuwakilisha ka li na le kama ni li jitu kama vile kosa lake kubwa sana
 
Ukienda baadhi ya nchi za ulaya na Marekani ukaenda kanisani na misikitini utakuta wazee na watoto.
Vijana wapo busy kutafuta shillingi.Nilimuuliza mmoja akaniambia utamuabudu je MUNGU ukiwa na njaa? Natatufa kwanza nikipata wakati huo nitakuwa mzee najenga kanisa kisha namrudia MUNGU lazima atanisamehe tu.
 
Hii dini ikija kisawa sawa nitakuwa wa kwanza kuingia maana maneno yaliyoko kwenye Agano la Kale na manabii ni wale wale walitajwa kwenye Qoran.Tulitofautiana pale kwa Ibrahim kwa mkewe Sara na kijakazi Hajra.
Halafu katiba ya kidunia nayo iingizwe kwenye huo msahafu wa hiyo dini mpya mfano haki sawa na sikiliza maoni ya wananchi na usijilimbikizie mali ukiwa kiongozi mkubwa.
Zile amri kumi za MUNGU zilizokwenye biblia nazo zote ziingizwe.MUNGU huyu tunayemuabudu wote atakuwa ni yule yule.YESU na Mohamed wote tutakuwa tunawaabudu kama kawaida.
 
Kuna masheikh wa mitandaoni wanaserebuka kwa nyimbo za mapambio ya kumsifu Mungu, hawana ubaguzi katika kusifu na kumuabudu Mungu. Wamekuwa kama wasamaria wema kwa jinsi wanavyoonesha upendo kwa wengine
 
Ivi kwanini Wakristo mnapenda kuunganisha Uislamu na Ukristo?

Mimi naona mada kama hizi huletwa na Wakristo tu ila Muislamu anaejielewa na dini yake hawezi andika kama hayo uloyaandika mtoa mada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…