Dini na maadili, kisima kimekauka

Dini na maadili, kisima kimekauka

nzalendo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,106
Reaction score
12,916
DINI na MAADILI: Kisima Kimekauka.

Idara ya Falsafa na Maadili ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) kwa ushirikiano na Chuo cha Kanda cha Theologia na Biblia cha Kilutheri Nyakato - Mwanza, wameendesha kongamano kubwa.

Walinialika kama “Mropokaji” rasmi wa kongamano hilo lililohusu “Nafasi ya Dini katika kuchochea Maadili ya Kijamii na Amani”. Lilifana. “Mropoko” wangu katika mengi uliibua haya:

1. Ni dhana isiyo halisi kuamini kuwa dini ndiyo inayoshawishi maadili ya kijamii kwa sasa kwa sababu watu wengi hawakumbuki kiongozi wa dini kasema nini kabla ya kufanya maamuzi yanayohitaji maadili (sex, vileo, mahusiano, ndoa, mali, madaraka, nk).

2. Mitandao ya kijamii na watu maarufu (super stars na celebrities) wanatumiwa kama “role model” katika kufanya maamuzi binafsi.

3. Dini zote kuu zinasikilizwa na kuheshimiwa lakini haziongozi maamuzi binafsi ya waumini:

-Dhehebu langu linakataza “kumwagilia moyo” lakini waumini wanamwagilia kweli. Jumapili ukiwaona kanisani utadhani hata harufu ya urabu hawajawai kuisikia.

-Dhehebu fulani linazuia uzazi wa mpango lakini waumini wake ndio watumiaji. Ukiwaona jumapili wanavyoshangilia mafundisho ya kutotumia uzazi wa mpango, utadhani hawatumii.

- Dini fulani inazuia kula kitimoto, nilienda nchi fulani ambayo 99.9% ni waumini wa dini hiyo, nikapelekwa mtaa fulani nikakuta siyo wanakula tu, bali wanabugia!

-Ushoga na ndoa za aina mbalimbali (na wanyama, na watoto wa kuzaa) zinaongezeka katika nchi zilizokuwa za kidini (State churches au State religion).

4. Barani Afrika, Ukristo na Uislam ni kama dini za halaiki kwa ukuaji wake. Mahekalu hayatoshi kwenye sikukuu mpaka ibada zifanyike viwanjani vya mpira. Lakini:

- Rushwa, ufisadi, vita, umaskini, ukatili, mauaji ya kimbari na dhuluma vimezagaa kwenye meza za watawala mpaka uvunguni mwa vitanda. Viongozi wa nchi ni wakristo na waislamu!

- Imani za kishirikina na matumizi yake katika siasa, michezo, dini, biashara, taaluma na ndoa vinaongezeka. Yaani eti msomi anaamini kuweka mfukoni kidole cha Albino, atamiminiwa kura hata kama kichwa ni kitupu?!

5. Kuibuka kwa dini zinazoosha ubongo (brain washing) badala ya kujaza ubongo kwa maarifa (reasoning). Watu wanashawishiwa kumfuata mtu badala ya kumfuata Mungu au watu wanaacha taasisi dini kumfuata mtu binafsi.

Kisima cha maadili (Dini) kimekauka. Tupate wapi mbadala wa kuhamasisha maadili.
Tuliwasikiliza waislam
Tukawasikiliza Wahindi
Tukawasikiliza Rastafarians
Tukawasikiliza wakristo (RC)
Tukawasikiliza wa dini za asili (ATR)
Kisha tuksmsikiliza “mropokaji rasmi” aliyechambua dini, siasa na serikali.

Tuko vibaya lakini tunasema “tuko vizuri”.

Kauli mbiu ya kufunga kongamano, UCHAWA SI UTANZANIA. Bishop Dr Benson Bagonza (ELCT )
 
Back
Top Bottom