PS: Majibu yangu yote ni kwa msaada wa ChatGPT 4
KWELI
Maana yana 'fasaha na koherensia ya hali ya juu'.
Kwa kuongezea, Mashariki ya kati na Uajemi kuna mengi ya kiutamaduni na imani, tena yaliyofaulu 'marefu sana ya maisha'...
Ikiwa watu wengi watachunguza vizuri mambo na habari za watu kutokea huko, wasije kushangaa hata mengi wanayoyajua katika 'Mapokeo ya Dini kubwa', za leo, pia yana vionjo vya kale vya tamaduni za Misri na Mashariki ya Kati.
Alama zote za Dini kwa mfano tuseme
Mwezi na Nyota,
Msalaba ama hata pia
Nyota ya Daudi ni urithi wa 'Ujuzi wa Kiimani' wa Watu wa Zamani --zamani khasa ya Misri na Mashariki ya Kati, kungine Duniani ama na
hata nje ya Sayari ya Dunia; wakati wa nyuma kupita ukadirifu wa kuja kwa dini zenyewe kubwa za hivi leo na tena hata kuhusishwa na wale wanaotajwa katika dini kuhusikana--tuseme kwa mfano '
msalaba na Yesu'.
Druze ni mapokeo ya 'Ujuzi wa Kiimani'...
Karne ya 20,
George I Gurdijieff na watu wake, akiwepo
P D Ouspensky, walishiriki baadhi ya
'Ujuzi' na 'Mambo' ya Hekima za Mapokeo Udruze...
GI Gurdijieff, kutamkwa kana 'G I Gujifu', mwenyewe alikuwa ni mtu aliyekutana, kufunzwa na kufundwana na jamii ya wengi wa watu wa 'Maarifa na Maarifu'--wakiwemo '
Madaruweshi wa Kisufii'.
Masufii ni watu wa '
Maarifa na Maarifu' na kutokea kwenye jamii tofauti tofauti ya Magharibi ya Afrika na Mashariki ya Kati; ujuzi wao mambo na maarifa ni sehemu ya 'Ujenzi wa Jumuiya za Imani' za faragha kwa kuwa, 'Maarifa' huleta nasibu ya '
Uautokrati'--Maarifa ya Kweli huinua watu kimadaraja ya Utu na Utamaduni; kwa hivyo yanaweza kuwa na 'siri ya uhifadhi' ama 'Siri ya Mageuzi ya Sura za Wanajamii'--Jambo ambalo huamuliwa na wenyewe wenye 'Maarifa'; na si jamii ama umma usiyo kwenye kujua ilivyobora.
Masufii wa '
Mtingo Nakshbandi' kwa mfano, ndiyo mafundi wa nakshi na urembo unaohifadhi 'Hekima' ya 'UTU Bora'. Ukiona Msikiti, ama jengo la Umma kukusanyika kwa ibada, limejengwa na sanaa na urembo fulani mahsusi,
matumizi ya rangi ya kijani, basi ndiyo ifahamike kuna 'Maarifa yamehusika'... Mambo kama vile Ujenzi wa
MInara na Madungurushi, ama '
pembe mstatili' juu ya majengo ya ibada vyote ni 'Maarifa'...
Vivyo hivyo
ujenzi wa Makanisa na Kathedrali kuwa na
michongoko ya 'Msalaba'--mambo ya
milango mitatu, mambo ya
Vioo vya Rangi rangi, 'mistatili wima ya kiujenzi' ni mambo ya 'Maarifa'.
Kwa hivyo ipo namna ya kubaini uwepo wa 'Watu wa Maarifa' nyuma ya dini zote, jamii zote na nyakati zote; watu hawa daima wanafanana kwa 'dhamira', 'matendo' na 'faragha' zao... Hawa wote huongozwa na kitu kimoja; Utumishi na Uteule kwa '
Umma unaojitafuta maana ya kuishi/Uisho' na '
pambazuko la kiroho'...
View: https://www.youtube.com/watch?v=UKPwZqUUrQo