Dini ya Uislam inaruhusu kufuga mbwa nyumbani?

Kwa ulinzi/uindaji ni ruhusa kufuga ila kwa kutunia kunyonya kipapa ni kharam.
 
Kuna mmoja anafuga nguruwe tukimuambia yeye ni muislamu anasema dini haimletei mboga nyumbani kwake pia anasema yeye anafuga ila HALI NGURUWE yeye anataka pesa 🤣🤣🤣

Sasa huyo ni mtu binafsi. Usichanganye dini ya uislamu na muislamu. Dini ya Uislamu ipo sahihi na imekamilika ila sisi waislamu tuna mapungufu. Hayo ni mapungufu ni ya kila mtu na yasihusishwe na dini yetu
 

Angalia hii clip


View: https://youtu.be/Ik-IX0-1XX0?si=xmAf1bk5QgC-0gJs
 
Mbona wema anaishi nae na kumfanya mwanae ...na msikitini anaenda
 
Ww fuga bana haya mambo mengine ni unyanyapaa tu wa viumbe vya Allah wetu..!!

Mbwa ukimtunza vizuri wala hana shida, ni rafiki mzuri sana wa binadamu na mlinzi kuliko hata paka, vi nyau waga vina mashauzi sana wakati umuhimu wake ni mdogo nyumbani, ila vinapewa treatments ambazo mbwa ndo anapaswa kua priority kupata hizo treatments...
 
Tuliletewa mdada wa kazi kavaa nikab kabisa, alivyofika uso aliacha wazi. Kuambiwa kuna mbwa akasema hatoweza kuishi hapa. Tukamwambia atakuwa anampikia tu, vyombo vyake tutaosha wenyewe. Akasema yaani sehemu/sakafu anayopita mbwa hawezi kukaa. Akageuza saa hiyo hiyo.
 
wanacho nichekesha kuwa dini yao ni kasoro wapo na uwezo wa kufuga simba,chui na paka ila hawajui wote kuwa ni jamii pamoja na mbwa.
dini ni dalili za ukichaa
Pundamilia ni halali kula ila punda wa nyumbani haliwi.

Na hao uliowataja ni cats na mbwa si katika wao, wakati watu wanasoma shule wewe ulikuwa busy kusugua mbegu za ubuyu sakafuni kuunguza wenzako.
 
Ninachojua sheria zimewekwa ili zivunjwe.... Niko na rafikiangu kila wakati ni kanzu na barakashia lakini uchumi wake unatokana na ufugaji wa nguruwe
Mada inahusu kufuga mbwa Ni halali au haramu.
Suala la nguruwe Hilo linajukana na limeshashindikana, na hitimisho Ni kwamba kula ili usife.
 
Uislamu una muongozo gani wa kidini katika kufuga mbwa wa ulinzi au kama mnyama kipenzi(pet) na kuishi ndani ya nyumba?

Hali ya ufugaji mbwa Uarabuni ikoje?
Uislamu unaruhusu kufuga mbwa kwa ajili ya ulinzi na hata usaidizi wa kazi kama uwindaji kwa utaratibu maalum wa kuwa na mipaka katika kuishi nae. Suala la kufuga mbwa as a pet uislam hauentertain such practice..
 
yaani unashangaa mbwa kuwa shetani ..hata baadhi ya binadamu ni mashetani
 
Swali langu: kuna uhusiano gani kati ya mate hayo ya mbwa na sala? Na kingine kama ni swala la rubela tayari kwa sasa tuna chanjo na huo ugonjwa ushapotea kabisa.

Hayo mate ya mbwa na ngozi ya nguruwe ni moja wapo ya najisi ambazo inabidi zisafishwe kwanza kabla ya kusali. Kumbuka uliuliza najisi ni nini nikakujibu hapo juu, kama hujaelewa unaweza tena kuuliza tu usiwe na shaka.

Katika uislamu sala ina masharti maalumu ili iweze kuwa sawa kwa mfano.
1. Ni lazima uwe msafi yani usiwe na najisi mwilini mwako na kwenye nguo zako
2. Ni lazima uchukue udhu/ kutawadha kabla ya kusali
3. Ni lazima uelekee kibla
4. Kila sala yenyewe ina muda wake maalumu

Usipotimiza sharti hata moja sala yako itakuwa haipo sawa
 
Shekhe acha matusi! Unasema nguruwe akimgusa mtu ni najisi wakati sisi tunamla?
 
Kwani Uislam unasemaje kuhusu hili? Na tokea lini Waislam "matajiri" wakawa ndio Uislam wenyewe?
Ametania tu, Mwijaku sio tajiri lakini anafuga mbwa kama pet.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…