Dini ziachwe na ziheshimiwe

Dini ziachwe na ziheshimiwe

Mjanja M1

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
4,058
Reaction score
14,382
Mimi Mjanja M1 siamini dini yoyote ulimwenguni lakini haimaanishi kuwa sitaki dini ziwepo ulimwenguni.

Nimekaa na kutafakari sana endapo kama huu ulimwengu ungekuwa hauna Imani za dini ingekuaje, jibu nililopata ni kwamba binadamu tungeishi kama Wanyama.

-Watu wangezaliana hovyo na hata kushiriki tendo na ndugu zao.

-Watu wangedhurumu wenzao kwakuwa wanaamini hakuna hukumu huko mbeleni.

-Watu wangeuana na kufanyiana unyama bila ya kujali lolote.

-Malezi ya familia yangekuwa hamna (Kizazi kilichopotea) n.k

Namalizia kwa kusema, NI MPUMBAVU PEKEE NDIO ATAPINGANA NA HILI BANDIKO HADHIMU.

Uzi Tayari.

Mjanja M1 kwasasa napatikana Berlin Germany 🇩🇪
 
kabla ya dini za Wazungu na Waasia watu walikuwa hawaoani ndugu kwa ndugu, wazee walifahamu mema na mabaya, japo walijisitiri kwa ngozi kulikuwa na maadali, kuheshimiana na magonjwa hayakuepo ya kijinga.

Ona leo hii kubakana kwingi, mapenzi ni hela , kusali ni hela na kama huna hela huna maana hata wanaoeneza dini hawakuziki, ubaguzi kwa kila kona, ukitaka huduma kwenye dini za kizungu hela.

Dini zetu za asili eti ni za kishenzi.

Sijajua mleta uzi unazungumzia dini zipi? Jibu niendeleze hoja haraka sana.
 
Back
Top Bottom