Dira: Bunge maalamu la katiba

Dira: Bunge maalamu la katiba

autorun255

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2013
Posts
1,105
Reaction score
364
Najua wengi tutakuwa tumefuatilia yaliyojili ndani ya bunge la katiba.

Imekuwa ni siku moja tu lakini nimejionea mengi kutoka kwa wajumbe wateule.

1. MAHUDHURIO
Bunge lilianza kwa kuwepo viti vingi vikiwa wazi.

2. UCHELEWAJI KWENYE VIKAO
Ni pale kulipotokea kuzidi kura zilizopigwa kuliko idadi ya wabunge waliohesabiwa. Yawezekana kuna waliochelewa kuingia bungeni.

3. NIDHAMU
Utadhani hawakupatiwa semina namna ya shughuli za kibunge zinavyoendeshwa. Wajumbe wanalopoka lopoka hovyo.....
Hapa imekaaje hii au ndo wamejifunza kutoka kwa wabunge teule....
Vile vile kutoheshimu kiti.

4. KUKOSA UVUMILIVU
Walipo elezwa kurudiwa shughuli ya kupiga kura......hapo sasaaa
Maoni mengi yalikuwa kuharakisha zoezi liishe kila mjumbe akuchukue 300000 faaaasta. Hiki ni kiashilia jinsi mchakato utakavyokuwa hapo mbeleni kwenye vifungu na ibara kuharakishwa kupitishwa ili muradi tu siku iishe.

Nnavyoona mimi , Kama hali yenyewe ndo hii , sidhan tutapata katiba bora .


Je tutaipata katiba tunayoitarajia??????
 
Wale jamaa zangu wa chama fulani wanangojea siku ya kupinga serikali tatu watajaa haoooo!! siku hiyo hata mama nitilie watafanya biashara. Pesa yote hiyo waliyopangiwa nafikiri tuombe katibu wabunge afanye mrejesho kila siku tujue wangapi hawajahudhuria ili pesa yetu irudi hazina tununulie vitabu vya watoto wetu mashuleni hasa shule za kata
 
Kutegemea kuwa bunge la katiba litafanya mambo tofauti na bunge letu la kutunga sheria ambalo limejaa mipasho ni kutegemea kupata jibu tofauti wakati unatumia njia ile ile kupata ufumbuzi wa tatizo!! Haiwezekani kupata katiba itakayokidhi mahitaji ya waliowengi kwasababu chama tawala ambacho kina wanachama wasiozidi milioni tano kati ya wananchi milioni arobaini na tano ndio chenye idadi kubwa ya wajumbe ambao ndio watakaopiga kura ya kuamua ni aina gani ya katiba wanayoitaka!!! Katika kuhakikisha kuwa kura ya maoni pia inathibitisha mapendekezo yao ; ccm watahakikisha kuwa vyombo vya dola vinathibiti upigaji na uhesabuji wa kura ili waibuke washindi!!! Zoezi zima limetumia fedha nyingi lakini matokeo yake hayatakuwa na manufaa kwa walio wengi na hivyo kuashiria vurugu kubwa nchini huko mbele.
 
Hili ni tatizo la kitaifa lililotufikisha hapa. Inakuwaje chama chenye wanachama pungufu ya milioni tano kuamulia watu milioni arobaini na tano. Hawa watu wazima na vijana sema milioni ishirini na tano kwa kukisia walikuwa wapi wakati wa kupiga kura? Au walikipigia kura chama tawala? Kama ndivyo hakuna haja ya kulalamika. Lakini kama hawakupiga kura huo ni uzembe inaowapasa kuubeba katika kipindi cha maisha yao kilichobaki. Hakuna maana ya kuongelea vurugu wakati kura yako moja unayo lakini wakati wa uchaguzi aidha hukujiandikisha au hupigi kura au ukipiga mnazitapanya kwa utitiri wa wagombea wa vyama vya upinzani. Kubali matokeo tu sasa tusubiri tuone.
 
Back
Top Bottom