Dira na Maono ya Taifa ni mali ya watanzania

Dira na Maono ya Taifa ni mali ya watanzania

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Maono ya taifa ni dira inayofafanua malengo makuu ya nchi kwa muda mrefu. Ni muhimu sana maono haya yatoke kwa wananchi wenyewe, kwani wao ndio wahusika wakuu na walengwa wa maendeleo.
images (63).jpeg


Makala hii inajadili wa ufupi tu sababu za kwa nini wananchi wa hali ya chini wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuandaa dira na maono ya taifa, huku Wajumbe na wawakilishi wa Bunge wakiwa waangalizi tu.
images (64).jpeg


Kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya dira na maono ya taifa katika maisha ya Wananchi: Wananchi ndio wanaopitia changamoto za kila siku, sio Mwigulu wala Mchengerwa, ni wananchi wa huku mitaani ndo wana ndoto, matumaini, na wanajua changamoto msingi zinazowakabili.
images (69).jpeg


Ni kitu kigumu kuamini kuwa Mhe. Ndumbaro anafahamu kwa kina ndoto za wanasongea kuzidi wana Songea. Kushiriki kwao katika kuandaa maono na dira ya taifa kunahakikisha maono hayo yanajibu mahitaji yao halisi na yanazingatia mazingira yao ya kila siku.
images (72).jpeg


Maono yanayotokana na wananchi yana nguvu zaidi kimaadili na kisiasa kuliko yakitoka kwenye kinywa cha mwakilishi wao. Wananchi wanakuwa na hisia yaUmiliki na wako tayari kushiriki katika utekelezaji wake. Hii inaongeza uwajibikaji wa serikali na taasisi nyingine katika kufikia malengo yaliyowekwa.
images (68).jpeg


Ni sawa na wakati ule ambao wananchi walimbadilikia Mbunge wao, Mhe. Charles Mwijage, Mbunge wa Muleba Kaskazini, huyu ndio ulidhani anaweza kuwaongelea wananchi wa Kata za Mayondwe, Fumbo pamoja Ruhanga? Wananchi waliona isiwe kazi sana hivyo kumpa haki yake.
images (70).jpeg


Demokrasia Shirikishi, kwani kuwashirikisha wananchi katika kuandaa maono na dira ya taifa ni utaratibu muhimu wa kuimarisha demokrasia shirikishi. Wananchi wanapata fursa ya kutoa maoni yao, kujadili changamoto, na kupendekeza njia za kuboresha maisha yao.

Hii inaongeza imani yao katika serikali na utaratibu wa kidemokrasia. Sio afya kuona watu 393 wakiamua mambo makubwa ya taifa la watu zaidi ya milioni 65.5 huku tukiwa na kumbukumbu nzuri ya watu hawa 393 kuingiza chaka taifa, sio kwenye Tegeta Escrow wala sio kwenye Bandari.
images (67).jpeg


Ni vyema wananchi wakaanza kupewa kipaumbele kwenye kuamua haya mambo kuliko kuweka rehani maisha ya watanzania zaidi ya milioni 65.5 mikononi mwa watu 393, sio afya hata kidogo.
images (65).jpeg


Wananchi wanatoka katika tabaka mbalimbali na wana uzoefu tofauti, ndani ya jamii kuna watu wenye maarifa mbalimbali, wapo ambao wana uwezo wa kudadavua ambo pasipo kuwa na shauku la kutafta nafasi serikali, wapo pia wenye kutamani kuna siku moja watu wataishi kwa amani pasipo kuwa na hofu ya kuitwa na TRA na siku chache baadaye ndugu zake kukuta maiti ipo mochwari.
6576e5b1b5b3e3143c220ee2bf6504177f43375dba5af.jpg


Kuwashirikisha wananchi kunaleta utajiri wa mawazo na mitazamo ambayo inaweza kuboresha maono ya taifa, sio kitu chenye afya kwa taifa kuona watu wachache, yaani asilimia 0.0006% ya idadi yote ya watanzania wanakubaliana jambo na linafanyiwa kazi?
images (71).jpeg


Maono yanayoandaliwa na wananchi wenyewe yana uwezekano mkubwa wa kuwa endelevu kwani yanazingatia mahitaji ya sasa na ya vizazi vijavyo kwa kiasi kikubwa. Mtanzania ambaye yupo na familia yake huko Kijiji cha Mongomongo unadhani ukimuuliza kuhusu hii mada atakupa majibu sawa na na Mhe. Hamida Mohammed?
images (64).jpeg


Je unadhani maisha ya kila siku ya vitongoji vya Mtohutohu na Mang’ang’a yanazungumza lugha sawa na Hamida? Sidhani kama kuna Mbunge ambaye anaweza kuongea kuhusu shule kukosa matundu ya vyoo kama hana mtoto wake anasoma shule hiyo.
images (72).jpeg


Mhe. Mwigulu ni Mbunge wa Iramba Magharibi, je unadhani anaweza kumpeleka Isack akasome Shule ya msingi Tutu? Halafu Mhe. Mwigulu ndo aende kuishauri serikali namna bora ambayo Iramba itafanikiwa kielimu?

Ingawa ni kweli kuwa wajumbe wa Bunge wana jukumu muhimu la kuwakilisha wananchi, kuna sababu kadhaa kwa nini hawapaswi kuwa mstari wa mbele katika kuandaa maono na dira ya taifa:
images (66).jpeg


Wabunge mara nyingi wana maslahi ya kisiasa ambayo yanaweza kuathiri utaratibu wa kuandaa maono. Wananchi wanaweza kuwa na uhuru zaidi wa kutoa maoni yao bila woga wa upendeleo wa kisiasa.

Mara kadhaa tumeona kuwa wabunge wengi wa CCM wakiwa wanazungumzia miradi ya serikali wakitumia maneno “ILANI YA CHAMA” hivyo kutengeneza dhana kuwa chama ndo kimepeleka maendeleo mradi wa maji sehemu fulani ilihali pesa iliyotumika ni kodi ya wananchi.
images (73).jpeg


Hautochelewa kusikia kuwa vipengele kadha wa kadhaa ndani ya dira ya taifa ni sehemu ya Ilani ya chama, wakati taifa sio sio kwa ajili ya CCM, CHADEMA wala CUF.

Wabunge wanachaguliwa kwa muda mfupi sana na utumishi wao una kikomo, ila dira na maono ya taifa yanapaswa kuwa ya muda mrefu na hayapaswi kubadilika kutokana na mabadiliko ya kisiasa ya muda mfupi. Kwa mfano Ilani ya CCM ikibadilika haina maana tubadilishe na dira kwa kigezo tu CCM ipo madarakani na Rais anatoka CCM.
images (74).jpeg


Je 2025 Rais akitoka CUF ina maana tubadilishe dira na maono kuendana na Rais anayetoka CUF? Watanzania zaidi ya miloni 65 wafuate matakwa ya mtu mmoja? Ukizingatia mihimili miwili tayari ipo chini ya mhimili mmoja. Dira na maono ya taifa sio maono ya Dkt, Nchimbi wala Mhe. Mnyika, ni suala nyeti ambalo halihitaji mzaha.
images (71).jpeg


Kwa bahati mbaya sana, kumekuwa na changamoto za mara kwa mara za uaminifu miongoni mwa wanasiasa wenyewe. Wananchi wanaweza kuwa na imani zaidi na maono yanayoandaliwa na wao wenyewe kwa sababu mara kadhaa wananchi huzungumza lugha ambayo ndo wanaishi.

Peter Msigwa alipokuwa ni CHADEMA lia lia kabsa na mkosoaji mkubwa wa sera za CCM ila sasa hivi ni kada na mwananchama kindakindaki wa CCM, Mwita Waitara ilikuwa vivyo hivyo.

Kuna njia mbalimbali za kuwashirikisha wananchi katika kuandaa maono ya taifa:

Mikutano ya Umma: Kufanya mikutano ya umma katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kuwapa wananchi fursa ya kutoa maoni yao.
Vyombo vya Habari: Kutumia vyombo vya habari kama vile redio, televisheni, na magazeti kuhamasisha mjadala wa umma kuhusu maono ya taifa.
images (69).jpeg


Mitandao ya Kijamii: Kutumia mitandao ya kijamii kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwaruhusu kutoa maoni yaoMtandaoni.
Kuwashirikisha wananchi katika kuandaa dira na maono ya taifa ni jambo la msingi kwa maendeleo endelevu ya Tanzania. Wananchi wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika utaratibu huu, huku Wabunge wakiwa waangalizi tu.
images (68).jpeg


Hii itahakikisha maono ya taifa yanajibu mahitaji ya wananchi wenyewe, maono yenye uhalali, na yenye uwezekano mkubwa wa kutekelezwa kwa mafanikio.

NB: Dira ya taifa ni kwa ajili ya watanzania sio kwa ajili ya Rais wala viongozi! Kiongozi ataondoka na hata kufariki ila Tanzania ipo mpaka kesho.
 
Rulers Class
Specialized Class ( Wabeba Mizigo ya Raia / Watumishi waajiriwa ).
Bewildered herd ( Raia )
Yaani hujui unachotaka na huna Maamuzi zaidi unaonwa mpiga kelele.

Dira ya vikao vya ccm ndio dira ya nchi kwahiyo tulipo na tunakoenda ni Matokeo wa Yale wanayojadili Sinktank yeah sinkiz wa Chama hicho.

Angalia tulipo Kama Nchi angalia walipo wao mmoja moja Kama Watumishi na Watawala utagundua wamefanikiw kuendeleza zaidi Mambo Binafsi kuliko Miradi na kazi walizopewa kwenye Ofisi za Umma.

Hata kile wamekinadi Kama Dira ya Taifa huoni Cha maana utadhani walikuwa wakiongelea Taifa Soap.
 
Rulers Class
Specialized Class ( Wabeba Mizigo ya Raia / Watumishi waajiriwa ).
Bewildered herd ( Raia )
Yaani hujui unachotaka na huna Maamuzi zaidi unaonwa mpiga kelele.

Dira ya vikao vya ccm ndio dira ya nchi kwahiyo tulipo na tunakoenda ni Matokeo wa Yale wanayojadili Sinktank yeah sinkiz wa Chama hicho.

Angalia tulipo Kama Nchi angalia walipo wao mmoja moja Kama Watumishi na Watawala utagundua wamefanikiw kuendeleza zaidi Mambo Binafsi kuliko Miradi na kazi walizopewa kwenye Ofisi za Umma.

Hata kile wamekinadi Kama Dira ya Taifa huoni Cha maana utadhani walikuwa wakiongelea Taifa Soap.
Tunapoelekea maono ya Mama Samia ndio yatakuwa maono ya kila mtanzania! Je maojo ya mtu mmoja yanaweza kuwa sawa na watu milioni hamsini!?
Inafikirisha sana!
 
Back
Top Bottom