UTANGULIZI
Hapa nchini Tanzania kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa wasomi hasa wanaohitimu ngazi ya chuo ambapo wanategemea kuajiriwa kutokana na walichokisomea. Ofisi ya Takwimu Tanzania 2020/21 ilionesha kuwa jumla ya watu 675,899 (2.8% ya watu wenye ajira) ni waajiriwa serikalini. Takwimu za TCU 2009/2010 hadi 2020/2021 zinaonesha kuwa kufikia mwaka 2021 kulikuwa na jumla ya wahitimu wa chuo kikuu 490,390. Takwimu hizi zinaonesha uhaba wa ajira serikalini na ongezeko la wahitimu vyuo vikuu bila kujumlisha wale wa vyuo vya kati.
Upungufu wa ajira hutokana na mambo mbalimbali ikiwemo; kukosekana kwa dira imara kwa wanafunzi tangu elimu ya msingi; vyuo kutoeleza kwa kina jinsi mhitimu anavyoweza kuajiriwa maeneo tofautitofauti au kujiajiri kutokana na programu au kozi anayosomea; na kukosekana kwa fedha kama kianzio cha ujasiriamali baada ya kuhitimu. Ukosefu wa ajira umefanya vijana kuanza maisha upya ya utafutaji bila kujali walichosomea. Kwa waliofanikiwa kupata mitaji wamekuwa wafanyabiashara na kuachana na swala ajira kabisa kwa kukosa tumaini. Ikumbukwe watanzania wengi hutumia miaka isiyopungua 16 kupata shahada ya kwanza ambapo elimu isipomfaa ni sawa na uwekezaji wa miaka 16 bila matunda.
MAPENDEKEZO YA KUONGEZA AJIRA KWA WAHITIMU WA VYUO
1. Kuanzishwe somo la utumishi wa umma kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu.
Somo hili litalenga kuwafanya wanafunzi wajue aina mbalimbali za watumishi wa umma na kazi zao, changamoto za kiutendaji, na mbinu za kujikwamua kiuchumi kupitia kada au kazi iliyosomewa. Somo hili itafaa sana likifundishwa na watumishi wa umma kutoka taasisi au maeneo mbalimbali ya kazi kwasababu Watumishi wanaweza kuwa na weredi mpana kuliko mwalimu mmoja kushinda anafundisha anachokielewa kuhusu wafanya kazi wa umma. Somo hili litasaidia pia katika kutengeneza dira ya elimu na ajira kwa mwanafunzi husika kwa kufahamu kiundani wafanyakazi katika sekta za umma na binafsi.
2. Wanafunzi wawe na dira ya elimu tokea ngazi ya msingi.
Dira ya elimu na ajira ni muongozo wa mwanafunzi katika safari yake ya elimu mpaka kuajiriwa/kujiajiri au vyote kwa pamoja. Dira hii itajumuisha shule atakazosoma, masomo/tahasusi atakayosoma, chuo na programu/kozi atakazosoma, na eneo la kuajiriwa/kujiajiri kadri ya elimu aliyopata. Rejea vielelezo 3 na 4 hapo chini.
3. Shule ziwe na tuvuti (website) kisha ziunganishwe kwenye tuvuti ya NECTA. Hii itarahisisha upatikanaji wa taarifa na uchambuzi wa shule. Taarifa za shule zijumuishe: historia ya shule; stadi na masomo yanayofundishwa; idadi ya walimu kwa kila somo; idadi ya wafanyakazi wengine kulingana na kazi zao; ada na michango ya shule; matokeo ya mitihani ya ndani, nje na kitaifa; na takwimu za maendeleo ya wanafunzi waliohitimu katika shule husika mpaka kufikia vyuoni na kujiajiri au kuajiriwa.
4. Serikali iruhusu kuchagua na kubadili shule za kusomea kuanzia shule ya msingi. Hii itawezesha mwanafunzi kupata elimu katika shule ya maono kupitia dira yake. Pia, hii italeta chachu ya ushindani kwa shule zote kuhakikisha zinatoa elimu bora na kupunguza kuhama kwa wanafunzi.
5. Wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne wapangiwe kusomea tahasusi (combination) au vyuo vya kati kulingana na walivyoomba kwenye kujaza form (SELFORMS) endapo watakuwa wamekidhi vigezo vya ufauru. Inawezekana mwanafunzi alifauru hesabu kwa daraja C huku Biologia ni A lakini ndoto yake ikawa ni kusoma hesabu, ndio maana kuna umuhimu wa kuangalia kile kilichoombwa kwa mara ya kwanza kwenye "SELFORMS"
6. Vyuo vitumie tuvuti zake kueleza kwa kina kuhusu programu/kozi zinazotolewa. Ufafanuzi uhusishe: vigezo vya kujiunga na programu/kozi; matarajio kwa mwanachuo baada ya kuhitimu programu au kozi husika; jinsi ya kuajiriwa/kujiajiri kwa maarifa ya programu/kozi husika; vyuo vinavyotoa elimu kwa ngazi inayofuata hadi PhD kwa kila programu; takwimu za wanachuo wanaosoma; takwimu za wahitimu katika chuo, walioajiriwa/kujiajiri na maeneo ya ajira. Pia viboreshe huduma kwa wateja mtandaoni kwa kila programu kuwasaidia wale wanaohitaji maelekezo.
7. Wahitimu vyuo vya kati na vikuu wapatiwe mikopo yenye riba nafuu mara wanapohitimu. Mikopo italenga kuinua ujasiriamali wakati wa kusubiri ajira. Mkopo utatumika katika utafutaji mpaka hapo mhitimu atakapopata ajira serikalini. Kwa wahitimu wa chuo kikuu walionufaika na bodi ya mikopo (HESLB), riba yao itakuwa sehemu ya kurejesha mkopo kwa serikali. Riba ya asilimia 5% inaweza kuwa rafiki.
8. Serikali inapochukua mikopo iangalie namna ya kubuni miradi mipya inayoendana na wasomi inao andaa ambapo hawa wasomi wataweza kujishikiza kwa maarifa waliyonayo. Mikopo ya serikali inayochukuliwa isilenge kuboresha tuu huduma za kijamii zilizopo bali kuwepo na miradi mipya kuongeza ajira kwa wasomi.
9. Waajiriwa wanaofikisha umri wa miaka 60 wastaafu ili kuongeza nafasi ya vijana. Ofisi ya takwimu za nchi (NBS) 2020/2021 ilionesha kuwepo kwa asilimia 6.1 ya waajiriwa wenye umri kuanzia miaka 65 wakati asilimia 27.1 ikiwa ni vijana wenye umri wa miaka 25-35. Kupungua kwa 6.1% ya waajiriwa wazee kutaongeza nafasi ya ajira kwa vijana ambapo na wahitimu wa vyuo huangukia humo.
HITIMISHO
Elimu yenye sababu na mantiki kiuchumi huanza na dira kwa msomi kisha mikakati ya serikali kumuwezesha msomi kujiajiri au kuajiriwa. Dira hii haiandaliwi na mtu mmoja bali mzazi, mlezi, ndugu, jamaa na marafiki na serikali kwa ujumla wanahusika katika kuiandaa na kuitabiri. Kubadilibadili muenendo kimasomo ni dalili za kutokuwepo kwa dira hivyo kuna kila sababu ya kuhakikisha dira inatengenezwa tangu shule ya msingi.
Somo la utumishi wa umma litalenga kumfanya mwanafunzi aelewe kinagaubaka matamanio yake tangu udogoni mpaka kufikia chuoni na kupata ajira. Ni rahisi kuipambania ndoto kuliko kupambania mabadiliko ya muda mfupi ambapo yamekuwa yakiwakumba wasomi katika hatua za sekondari ya juu, chuoni na hata kazini kutokana na kuwa hakukuwa na dira nzuri na uhaba wa elimu ya utumishi wa umma.
Kipindi cha kusubiri kuajiriwa kitaendelea kuwa kigumu sana endapo msomi hatakuwa na mawazo na fedha ya kianzio kufanya ujasiriamali au kuwa na mwanga wapi apate ajira katika sekta zisizo za serikali.

Kielelezo 1. Ajira za serikalini ni asilimia 2.8 ya waajiriwa wote Tanznia. Chanzo NBS Tanzania
Kielelezo 2. Jumla ya wahitimu chuo kikuu kufikia 2021 ni 490,390; Chanzo TCU

Kielelezo 3. Dira ya elimu na ajira kupitia shule na vyuo binafsi
Kielelezo 4. Dira ya Erimu na ajira kupitia shule na vyuo vya serikali
3. Shule ziwe na tuvuti (website) kisha ziunganishwe kwenye tuvuti ya NECTA. Hii itarahisisha upatikanaji wa taarifa na uchambuzi wa shule. Taarifa za shule zijumuishe: historia ya shule; stadi na masomo yanayofundishwa; idadi ya walimu kwa kila somo; idadi ya wafanyakazi wengine kulingana na kazi zao; ada na michango ya shule; matokeo ya mitihani ya ndani, nje na kitaifa; na takwimu za maendeleo ya wanafunzi waliohitimu katika shule husika mpaka kufikia vyuoni na kujiajiri au kuajiriwa.
4. Serikali iruhusu kuchagua na kubadili shule za kusomea kuanzia shule ya msingi. Hii itawezesha mwanafunzi kupata elimu katika shule ya maono kupitia dira yake. Pia, hii italeta chachu ya ushindani kwa shule zote kuhakikisha zinatoa elimu bora na kupunguza kuhama kwa wanafunzi.
5. Wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne wapangiwe kusomea tahasusi (combination) au vyuo vya kati kulingana na walivyoomba kwenye kujaza form (SELFORMS) endapo watakuwa wamekidhi vigezo vya ufauru. Inawezekana mwanafunzi alifauru hesabu kwa daraja C huku Biologia ni A lakini ndoto yake ikawa ni kusoma hesabu, ndio maana kuna umuhimu wa kuangalia kile kilichoombwa kwa mara ya kwanza kwenye "SELFORMS"
6. Vyuo vitumie tuvuti zake kueleza kwa kina kuhusu programu/kozi zinazotolewa. Ufafanuzi uhusishe: vigezo vya kujiunga na programu/kozi; matarajio kwa mwanachuo baada ya kuhitimu programu au kozi husika; jinsi ya kuajiriwa/kujiajiri kwa maarifa ya programu/kozi husika; vyuo vinavyotoa elimu kwa ngazi inayofuata hadi PhD kwa kila programu; takwimu za wanachuo wanaosoma; takwimu za wahitimu katika chuo, walioajiriwa/kujiajiri na maeneo ya ajira. Pia viboreshe huduma kwa wateja mtandaoni kwa kila programu kuwasaidia wale wanaohitaji maelekezo.
7. Wahitimu vyuo vya kati na vikuu wapatiwe mikopo yenye riba nafuu mara wanapohitimu. Mikopo italenga kuinua ujasiriamali wakati wa kusubiri ajira. Mkopo utatumika katika utafutaji mpaka hapo mhitimu atakapopata ajira serikalini. Kwa wahitimu wa chuo kikuu walionufaika na bodi ya mikopo (HESLB), riba yao itakuwa sehemu ya kurejesha mkopo kwa serikali. Riba ya asilimia 5% inaweza kuwa rafiki.
8. Serikali inapochukua mikopo iangalie namna ya kubuni miradi mipya inayoendana na wasomi inao andaa ambapo hawa wasomi wataweza kujishikiza kwa maarifa waliyonayo. Mikopo ya serikali inayochukuliwa isilenge kuboresha tuu huduma za kijamii zilizopo bali kuwepo na miradi mipya kuongeza ajira kwa wasomi.
9. Waajiriwa wanaofikisha umri wa miaka 60 wastaafu ili kuongeza nafasi ya vijana. Ofisi ya takwimu za nchi (NBS) 2020/2021 ilionesha kuwepo kwa asilimia 6.1 ya waajiriwa wenye umri kuanzia miaka 65 wakati asilimia 27.1 ikiwa ni vijana wenye umri wa miaka 25-35. Kupungua kwa 6.1% ya waajiriwa wazee kutaongeza nafasi ya ajira kwa vijana ambapo na wahitimu wa vyuo huangukia humo.
Kielelezo 5. Takwimu za NBS kuonesha 6.1% ni waajiriwa wenye umri kuanzia miaka 65
HITIMISHO
Elimu yenye sababu na mantiki kiuchumi huanza na dira kwa msomi kisha mikakati ya serikali kumuwezesha msomi kujiajiri au kuajiriwa. Dira hii haiandaliwi na mtu mmoja bali mzazi, mlezi, ndugu, jamaa na marafiki na serikali kwa ujumla wanahusika katika kuiandaa na kuitabiri. Kubadilibadili muenendo kimasomo ni dalili za kutokuwepo kwa dira hivyo kuna kila sababu ya kuhakikisha dira inatengenezwa tangu shule ya msingi.
Somo la utumishi wa umma litalenga kumfanya mwanafunzi aelewe kinagaubaka matamanio yake tangu udogoni mpaka kufikia chuoni na kupata ajira. Ni rahisi kuipambania ndoto kuliko kupambania mabadiliko ya muda mfupi ambapo yamekuwa yakiwakumba wasomi katika hatua za sekondari ya juu, chuoni na hata kazini kutokana na kuwa hakukuwa na dira nzuri na uhaba wa elimu ya utumishi wa umma.
Kipindi cha kusubiri kuajiriwa kitaendelea kuwa kigumu sana endapo msomi hatakuwa na mawazo na fedha ya kianzio kufanya ujasiriamali au kuwa na mwanga wapi apate ajira katika sekta zisizo za serikali.
Attachments
Upvote
5