Ndolezi Petro
New Member
- Jun 26, 2024
- 4
- 1
DIRA YA TAIFA 2050, HAKUNA AMANI BILA HAKI
Kwenye Mkutano wa Kongamano la Vijana la kuangazia Rasimu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050. Nilipatata fursa ya kutoa maoni juu ya kuboresha Shabaha za Dira.
Nilikwenda na hoja 7 mkononi kama ifuatavyo
01. Kuna Watanzania 91% ambao ni nguvu kazi ya Taifa walio nje ya mfumo wa Hifadhi ya Jamii kwa sasa ni 9% walio kwenye mfumo huu wa hifadhi ya Jamii
Tafsiri ya hii ni nini ?
Ni kwamba hawa 91% hawana kinga yeyote kwenye maisha yao ya kila siku. Wakumbwapo na majanga watajua wenyewe, wakati wa kujifungua mama mzazi atajua mwenyewe , Ukizeeka utajua mwenyewe maisha ya uzeeni hili ni kundi lisilo na uhakika wa leo na kesho yao.
Nimependekeza kwenye maboresho kwamba Dira iweke Shabaha ya kuwa na Hifadhi ya Jamii Jumuifu kwa makundi yote walio kwenye sekta rasmi na wale wapambanaji wa kila siku.
02. Msingi wa Dira ulioandikwa ni : Utawala, Amani, Usalama na Utulivu
Hoja yangu hapa: Hakuna amani bila Haki nilipendekeza Shabaha iandikwe "Utawala, Haki, Amani, Usalama na Utulivu
03. Juu ya ardhi kwenye matarajio 2050 imesema kila mtanzania awe na haki ya kumiliki ardhi
Hapa nimetoa angalizo sawa na Mwl. Nyerere alilotoa mwaka 1958 kama ilivyoelezwa kwenye kitabu cha Uhuru na Umoja kwamba " Tukiruhusu ardhi iuzwe kama kanzu basi ni kwa mda mchache Waafrika wachache watabaki na ardhi na wengi wao watakuwa watwana" alizungumza haya kwa muktadha wa Wakoloni wakati huo
Nami leo nazungumza kwa muktadha wa matajiri tukirusu ardhi iwe bidhaa sokoni basi masikini na vijana watabaki bila ardhi na yote itamilikiwa na matajiri
Pendekezo: Shabaha ya Dira iweke ulinzi wa kuwalinda watumiaji wa Ardhi wadogowadogo ambao ni Wakulima , Wafugaji n.k ili kundi hili lisije kuishi kama watumwa kwenye Taifa lao.
04. Dira imeweka Shabaha ya kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na Bima ya Afya na huduma Bora za Afya jambo jema lakini katika hili
Nimependekeza: Dira iweke Shabaha ya Bima ya Afya kwa wote isiyo na vifurushi kama ilivyo sasa. Hatupaswi kuwa na Bima ya Makundi kwani Kila Mtanzania anastahili kupatiwa matibabu bora ya Afya.
05. Juu ya ajira rasimu ya dira ya maendeleo imeweka shabaha isiyo na matumaini kwa vijana kuweza kutatua tatizo la ajira; kwani inasema angalau mtu mmoja katika kila Watanzania wawili wenye za kuajiriwa mmoja awe ameajiriwa kwenye sekta rasmi na wakiwa na mikataba kamili ya ajira.
Katika hili tafsiri yake ifikapo 2050 kila mwaka tutakuwa tunazalisha 50% ya wenye sifa za kuajiriwa kusalia mtaani na tutajikuta tunafika 2050 bila kutatua tatizo la ajira.
Nimependekeza: Dira iweke Shabaha yenye taswira ya matumaini kwa Vijana tuweke shabaha ya ifikapo 2050 tuwe tumefikia 80% ya wenye sifa ya kuajiriwa wawe na ajira rasmi. Tafsiri yake kila Watanzania 10 wenye sifa ya kuajiriwa 8 Wana ajira rasmi.
06. Dira imeweka shabaha juu ya kuwa na Katiba Imara lakini pia imeweka shabaha ya kuwa na serikali za mtaa imara ni jambo jema; lakini Katika kufanikisha hili kwenye rasimu ya Dira yote sijaona andiko lolote la Shabaha ya kuwa na mfumo huru wa Uchaguzi. Huwezi kamwe kupata viongozi imara wasiotokana na uchaguzi usikuwa huru na baraka za umma.
Nimependekeza : Kwenye Dira iongezwe Shabaha ya kuwa na Mfumo huru wa Uchaguzi
07. Hoja ya Mwisho kwenye rasimu ya Dira hakuna sehemu nimeona popote ILANI za vyama vya siasa ikitajwa. Tunatumia pesa nyingi za walipa kodi kutengeneza uelekeo wa Taifa letu lakini baada ya Uchaguzi Mkuu Dira inatupiliwa mbali chama kinachochukua Dola kinageuka kuimba wimbo wa tunatekeleza ILANI ya Chama.
Hapa nimependekeza Dira iweke Shabaha ya kuhakikisha ILANI za Vyama vyote zinajikita kuleta mawazo yao mbadala ni kwa namna gani watatekeleza Dira kupitia mpango wa miaka mitano mitano. Dira inapaswa kuwa msingi wa ILANI ya vyama vya siasa.
Mhandisi Ndolezi Petro
Waziri Kivuli Ofisi ya Waziri Mkuu-Bunge, Sera, Vijana , Kazi na Ajira ACT Wazalendo.
Dar es Salaam
19 Disemba,2024