ladyreen7
New Member
- May 29, 2021
- 2
- 1
Bado tunasafari ndefu
Na Binti Msakuzi
Kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo wananchi wanazidi kupoteza Imani na vyombo vya habari nchini. Kwa kiasi kikubwa wana haki hiyo baada ya tasnia hiyo kupoteza uaminifu kwa watazamaji na wasomaji wake. Maana huwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja, yupo atakeyetukuzwa kuliko mwingine na kwa hakika sio yule masikini.
Maamuzi ya kuchagua njia ya maslahi kati ya mwananchi na wenye nchi ndio yanaleta sintofahamu katika tasnia ya habari nchini. Vyombo vya habari binafsi hutegemea fedha za matangazo na mauzo ya kibiashara ili kumudu gharama, ambapo tenda hizo nyingi hutoka kwenye nchi. Je, unaweza kuukata mkono unaokuliasha? Fumbo la Imani.
Takwimu zilizochapishwa na Statista mwaka 2021 za kuonyesha kiwango cha umma cha kimataifa katika uaminifu wa makundi mbalimbali zimebainisha kuwa waandishi wa habari wanashikilia nafasi ya tano wakiwa hawaaminiki kiwango cha asilimia kumi. Ni Dhahiri kwamba Imani wa umma juu ya jamii inadidimia sanjari na kwa wanasiasa wanaoshikilia nafasi ya kwanza kwa asilimia 52.
Inaaminika kwamba vyombo vya habari ni miongoni mwa tunu zinazoweza kutumika kuchochea mabadiliko chanya katika jamii. Hii ni endapo itaibua matatizo yanayoikumba jamii katika harakati ya kutafuta ufumbuzi, jambo lililobaki kuwa ndoto kwa sasa.
Taswira ya uandishi wa habari kama taaluma yenye kuongozwa na miiko na maadili inapotea mara baada ya kuvamiwa na makanjanja. Hawa ni wale wanaoingia katika tasnia ya habari kama njia ya kujipatia posho kwenye mikutano ya habari. Ni aghalabu kuwaona wakijikita katika habari zenye maslahi ya jamii kwa madai ya kwamba hazina mashiko.
Safari ya mapinduzi katika tasnia ya habari ni ndefu sana nchini Tanzania. Hii ni kutokana na kutokuwepo kwa mfumo madhubuti wa kusimamia na kulinda ubora wa taarifa kwa wadau wa tasnia ya habari na maendeleo kwa kiasi kikubwa. Sababu mbalimbali zinadhorotesha tasnia ya habari nchini ikiwemo
Maslahi duni kwa waandishi wa habari
Vituo vya habari vimejificha katika mwamvuli wa kutumia waandishi wa kujitolea na mikataba yenye malipo duni kiasi cha kutokidhi mahitaji yao ya kila siku. Waandishi hao hujikuta wakikimbilia kazi za mikutano na vikao ambazo huwapatia posho inayowawezesha kusukuma gurudumu la maisha.
Ugumu wa maisha umewalazimu baadhi ya waandishi kuwa chawa kwa viongozi na wadau mbalimbali wanaohitaji mkono wa vyombo vya habari katika kufanikisha malengo hayo. Nyakati za uchaguzi zinazungumza mengi juu ya hili kwani viongozi wengi wa vyama vya siasa hujishikamanisha na waandishi wa habari kama ruba na kupe.
Tafiti iliyochapishwa katika jarida la The Richest inataja katika taaluma kumi zisizoaminika ulimwenguni namba nane na sita zinashikiliwa na vyombo vya habari na nafasi ya pili ikishikiliwa na wanasiasa. Inaelezwa kuwa uhusiano uliopo baina ya vyombo vya habari na wanasiasa ndio uliochangia kutokuaminika kwa tasnia ya habari.
Salumu* ni moja ya mwandishi wa habari wa gazeti jijini Dodoma kwa miaka mitano sasa. Anasema aliamua kuingia kwenye tasnia hii kutokana na ugumu wa maisha kwa kutumia elimu yake ya kidato cha nne baada ya kuambiwa kuna fursa kwenye kazi hiyo.
‘’Nilipoanza uandishi sikuwa najua chochote kuhusiana na kazi hii ila nikajifunza kila siku kwa wanaonizunguka. Habari za kijamii zinachukua muda kuziandaa na kugharimu nauli na fedha nyingine kukamilisha, jambo ambalo ni juu yako mwandishi na si ofisi. Muda mwingi nakimbizana na vikao na ziara kupata posho siku zisogee kwani mwisho wa siku wote tunasaka tonge’’
Miiko na taratibu za uandishi wa habari kutokuzingatiwa
Muongozo uliotolewa kwenye sheria ya huduma za vyombo vya habari ya 2016 kupitia waziri mwenye dhamana Nape Nauye ulibainisha kanuni inayowataka wanahabari kuwa na elimu kuanzia ngazi ya diploma ili kuendelea na tasnia ya habari. Utekelezaji wa kanuni hiyo ulitarajiwa kuanza mwaka 2022 lakini hakuna hatua yoyote iliyofanyika hadi sasa huku makanjanja wakiendelea kutamba.
Ukimya huo umeendelea kudhorotesha tasnia ya habari nchini katika ubora wa taarifa inayotolewa kwa watazamaji na wasomaji. Hali hiyo imepelekea kupata taarifa za matukio na si habari. Alisema,amesisitiza, amewataka, inatarajiwa ni miongoni mwa taarifa tunazozipokea kwa jina la habari kupitia vituo vya habari hivi sasa.
Msingi wa kupata habari za matukio yanayowagusa wananchi moja kwa moja umepotea kama inavyobainishwa na moja ya wana habari mkongwe mwenye miaka 24 kwenye tasnia hii. Dhana ya vyombo vya habari kuwa taswira inayoakisi maisha ya watu inapotea siku hadi siku.
‘’Zamani wakati tunaanza kazi kwenye tasnia hii ya habari umakini na umahiri ulikuwa ni wa kiwango cha juu. Tulitumia muda na nguvu kubwa kubainisha changamoto na kero za wananchi ili kupatiwa ufumbuzi na wenye mamlaka husika. Tofauti na sasa ambapo wenye nchi wanatumia vyombo vya habari kuwapa taarifa wananchi bila kauli ya mwananchi’’
Uhalisia huo unakuja baada ya wanahabari wengi kukosa weledi na misingi ya taaluma hiyo kwa kuamini kwamba ni kipaji pekee kigezo cha kuwa mwanahabari mashuhuri. Nafasi ya msingi ya elimu ya tasnia ya habari imepotezwa katika dira ya maendeleo ya habari. Hii ndiyo sababu baadhi ya vyombo vya habari vinapata wakati mgumu kuhimili mabadiliko ya teknolojia kwa kukosa ubunifu.
Tutarajie nini kwenye tasnia ya habari siku za usoni
Watu wanapopoteza Imani na vyombo vya habari hata ari ya kufuatilia taarifa inapotea. Vyombo vya habari vimejikita kuandaa taarifa na si habari kwa ajili ya mlengo wa taswira ya kidemokrasia na si uhalisia. Wananchi kutojiona katika habari hutilia shaka iwapo vyombo hivyo vina nguvu ya kuleta mabadiliko wanayoyatarajia.
Ulewa wa mtazamaji haupasi kupuuzwa wala kudhaniwa kwani mabadiliko ya tasnia ya habari yamewawezesha kubaini mbivu na mbichi. Kutiliwa shaka katika vyombo hivyo vya habari kunawaweka watazamaji na wasikilizaji katika mizani ya kuhoji mara mbili ukweli wa mambo yanayozungumzwa. Baadhi ya vyombo vya habari vitakosa Imani ya watazamaji wake kutokana na mlengo uliyojikita nao.
Nini hasa kifanyike
Kuna haja ya wadau mbalimbali wa tasnia ya habari kukutana na kujadiliana juu ya utekelezaji wa kanuni ya sharia za huduma za vyombo vya habari inayomtaka mwanahabari kuwa na elimu ngazi ya diploma na kuendelea kwa ajili ya fani hiyo. Pia kuzingatia maslahi ya malipo ya wanahabari ili kuepukana na rushwa hasa kutoka kwa wanasiasa. Muhimu zaidi ni kwa vituo vya habari kutenga fungu wezeshi kwa ajili ya kufanikisha habari zenye maslahi ya jamii.

Upvote
1