Dira ya Usalama wa nchi na wananchi wake...

Dira ya Usalama wa nchi na wananchi wake...

msemakweli10

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2013
Posts
229
Reaction score
46
Wana JF na wananchi wote Amani.

Nchi yetu ya Tanzania imekuwa ikisifiwa kuwa kisiwa cha Amani, watu wake ni wapole na wanyenyekevu.

Kutokana na utulivu uliodumu kwa takribani miaka 54 sasa, nchi yetu imekuwa ikikumbwa na majanga mbalimbali ya kidini na kisiasa.

Haitoshi kwa sasa nchi yetu inazoroteshwa na wachache wanaojiona wajanja na kuwaacha wananchi wakitaabika kwa matatizo yaliyo mengi ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Kwa sasa iliyobaki katika nchi yetu imekuwa ni kutafuta ni nani mchawi ashugulikiwe.

Swali la msingi limekuwa, ni kweli amekuwa akitafutwa mchawi au mchawi anafahamika ila zinatumika tu propaganda za siasa ili kuendelea kuvuna kilichopo?

Viongozi wetu kwa sasa wamekuwa wajanja na wameingia kabisa kwenye viatu vya wale wasomi wa kigiriki (sophists), kukandamiza tabaka la chini na kujiimarisha wao wenyewe.

Ni lini basi tutajitambua na kufanya maamuzi yaliyo sahihi kupata viongozi adilifu?

Karibu kwa mjadala
 
Tanzania hakuna dira ya kitu chochote; na kama ipo ni vigumu kuielewa na kutekeleza sio tu kwa waweka dira wenyewe bali hata kwa wawekewa dira na watekelezaji dira!

Ila kwa kuongezea kuna dira moja mathubuti na imara sana. Nayo ni kuhakikisha chama tawala kitaendelea kuwa madarakani iwe kwa kutumia nguvu ya dola ama kwa utashi wa wananchi. Vyovyote vile!
 
Back
Top Bottom