sir venance
Senior Member
- Oct 26, 2017
- 151
- 223
Wakati mwingine inabidi umsifie mtu kutokana na ubora wa kazi anayoifanya hata kabla hajafa..Hawa watu Kenny na Hanscana wanajitahidi sana katika kutengeneza music videos za bongo fleva kwa sasa, zamani tulikua na watu kama Adam juma na wengine ambao japo videos zao hazikuwa na quality zinazoeleweka ila walijitahidi kutokana na teknolojia iliyokuwepo,Sasa hivi tukiziangalia videos za muziki wa Tanzania tunaona utofauti kuanzia quality ya videos,story na ubunifu mwingine ambao unafanya videos zao ziwe nzuri,japo maeneo mengine mnaharibu kama kuweka rangi tofauti ktk kila eneo la video lakini kwingine mnajitahidi,angalau Sasa hivi tumewasahau watu kama Justin Campos, Godfather,sesan,Nick, Clarence peters,Moe mussa na wengine wengi ambao walikua wanafanya kazi nyingi za wanamuziki wa Tanzania,nchi yetu ina location nyingi nzuri kilichokua kinawapeleka wasanii huko nje ni quality, ubunifu na majina makubwa ya ma director wa nje lakini naamini hilo mmelifanyia kazi.