Director's speech

GP

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2009
Posts
2,049
Reaction score
161

Jamaa mmoja ambaye ni mkurugenzi wa kampuni moja kubwa ya
mawasiliano alikaribishwa kutoa speech katika tamasha moja la vijana
lililokuwa limeandaliwa kuhusu
kujiepusha na vitendo vyenye kuweza kusababisha maradhi ya
kisasa.Speech ya mkurugenzi huyu ilinukuliwa kama ifuatavyo;


"Hali ni ngumu sana vijana kwa sababu kila mmoja
anataka kuonja uzuri wa maisha ya kisasa. Mtandao wa
ugonjwa huu ni mkubwa,mimi nashauri muwe makini .
Jitahidini sana kukaa bila kupiga.

Ni muhimu simu zenu mzitunze sana na wala si kupiga piga kwani hii
gharama yake ni kubwa.Kama shida ya kupiga itakuwa kubwa, basi
hakikisha simu yako iko kwenye kipochi, na hivi vinapatikana kwa
wingi na gharama yake si kubwa.

Hii inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata madhara yanayoweza
kupatikana
kutokana na mionzi iliyoko katika simu hizi za kisasa.


Ni mwiko kabisa kupiga Voda kwa Voda kwani hii ina
hatari kubwa mno. Pia unashauriwa kutopiga tigo kabisa kwani hii inaweza kuharibu kabisa mfumo wa mawasiliano ya simu yako.

Watu wengi simu zenu zina fanya kazi vizuri tu na mna
hamu angalau ya kupibu, lakini hii nayo ni hatari,
kwani mwenzako akionyesha utashi wa kupokea ni rahisi
sana kwako kuamua kupiga kabisa.

Msifikiri mkikaa bila kupiga muda mrefu, eti simu zenu
zitamaliza chaji, hii si kweli.Hakikisha tu kwamba
simcard iko katika hali nzuri,hii ndio ina kumbukumbu
zote na ndio inaongoza mawasiliano yote.

Simu ni simu tu, na madhumuni yake yanafanana.
Usidanganyike na simu kuwa eti ina Kamera au double
skrini. Hizo ni mbwembwe tu.Kuna simu nyingi sana feki
siku hizi zinauzwa zimevishwa cover
mpya,usidanganyike.

Ukiona maisha bila kupiga hayawezekani, tafuta sehemu
inayoaminika na uwe unapiga hapo tu, hii inasaidia
sana kwani simu ukitumia peke yako inadumu zaidi
kuliko ile yenye subscribers wengi."

asanteni kwa kunisikiliza...

 
Speech kabambe, si ajabu hao vijana hawakuelewa kinachendelea.
 
Nna mashaka na huyo director kama anapiga sehemu moja tuu
 
Wengine hapo walidhani wanasikiliza promosheni maana siku hizi zero brain wako kibao
 
Huyo bila shaka ni dr ndodi wa haleluya sanitariam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…