Dirisha dogo limefungwa 2018

Dkileo

Member
Joined
May 23, 2017
Posts
51
Reaction score
46
Dirisha dogo limefungwa 2018

City wamemuongeza Aymeric Laporte…Niliwahi kusema City hawapo vizuri katika idara ya ulinzi..Huwa wanajilinda kwa kuishambuulia timu pinzani na kumiliki mpira muda mwingi wa mchezo..Kuja kwa Laporte kutafanya pep kufanya rotation ya beki wa kati mara kwa mara..Tumeona msimu huu Otamendi akicheza na Stones mechi nyingi..Kompany anasumbuliwa na majeraha mara kwa mara hivyo Pep alikuwa anabaki na Mangala ambaye alikuwa chaguo la nne..

Bado kuna mahali naona City wamepasahau..Bado napaangalia mahali anapo cheza Fernandinho…Endapo akiumia nadhani mbadala wake ni Yaya Toure ambaye sasa yupo hoi kwa kiasi Fulani..Toure naona hawezani na speed ya Man City ya sasa.Nadhani City walitakiwa kusajili mtu ambaye atakuwa mbadala wa Fernandinho

Man united wamemuongeza Sanchez..Nakumbuka niliposti kuhusiana na ujio na umuhimu wa Sanchez kwa Man united..Sanchez ni aina ya mchezaji ambaye alikuwa anakosekana katika kikosi cha Mourinho..Sanchez ni jeshi la mtu mmoja..Anafunga,ana assist pia ni mtu hatari katika mipira iliyokufa.United hawakuwa na mtu ambaye anaweza kuamua mechi haswa baada ya kuumia kwa ibrahimovic..Nadhani kwa Sanchez ,Jose amelamba dume..

Liverpool wamemuongeza Virgil van Dijk..Hakika hii inaweza kuwa solution sahihi kwa matatizo ya deffence ya Liverpool..Msimu huu Joel Matip,Dejan Lovren na Ragnar Clavan wamekosa uelewano kabisa..Livepool wamekua na tatizo kubwa la beki wa kati msimu huu..Nadhani Virgil anaweza kutengeneza combination safi na Matip..Lovren amekuwa na makosa makosa mengi msimu huu..

Nadhani tutammiss Coutinho…Haswa kwa chenga zake,assist na magoli yake ya nje ya box..bila kusahau faulo zake..

Barkley,Emerson na Giroud..Bado naona Conte anapata tabu sana msimu huu..Aliposajiliwa Morata niliandika kuwa bado sina Imani na Alvaro kum replace Diego..Nikasema msimu huu utakuwa mgumu kwa Alvaro haswa ukizingatia Alvaro sio mtu wa kutumia nguvu kama Diego..Alvaro ni mwepesi sana..Amekuwa akianguka mno uwanjani..Pia amekuwa akikosa nafasi nyingi za wazi…Giroud ni aina ya straika ambaye anatumia nguvu ..Tatizo la Olivier pia ni kukosa nafasi za wazi..Sina tatizo na usajili wa barkley…Pia ujio wa Emerson ni muhimu sana haswa ukizingatia Marcos Alonso anaonyesha wazi kuwa anahitaji kupumzika..

Bado tatizo lipo kwenye safu ya kiungo..Bakayoko ameshindwa kabisa kuziba nafasi ya Matic…Nilidhani labda Drinkwater angepata nafasi ya kucheza na Kante lakini naona Conte ameendelea kumtumia Zaidi Bakayoko..

Mikhi na Aubameyang..Hapa nadhani Wenger katumia akili mno…Bado nilikuwa nawaza Wenger kumpoteza Sanchez kwa kiasi kidogo cha pesa haswa ukizingatia mkataba wa Sanchez ulikuwa pungufu ya miezi sita..Hivyo kumpata Mikhi ,Wenger amekuwa mjanja sana..Pia Aubameyang ni straika mzuri sana..Ni mwepesi na anafanya maamuzi ya haraka mno..Japo wamempoteza Sanchez lakini kuwapata hawa wawili ni jambo zuri sana kwa Arsenal..Natamani sana kuiona combination ya Lacazette,Ozil,Mikhi na Aubameyang

Bado nakosa Imani na safu ya ulinzi ya Arsenal..Bado sjjua Kolasinac amekutwa na tatizo gani aseeeh

nicheki


youtube DEK sports & entertainment TV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…