Dirisha la usajili Tanzania kufunguliwa Julai 1 kufungwa Agosti 31, 2022

Dirisha la usajili Tanzania kufunguliwa Julai 1 kufungwa Agosti 31, 2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa taarifa rasmi ya dirisha kubwa la usajili kwa vilabu vinavyo shiriki ligi zote zilizopo chini ya shirikisho hilo la soka nchini Tanzania.

Taarifa hiyo itavihusu vilabu vyote vinavyoshirki ligi kuu ya NBC Tanzania bara,ligi daraja la kwanza (Championship), ligi daraja la pili ( First League) na ligi kuu ya wanawake Tanzania bara Serengeti Lite msimu wa mwaka 2022/ 2023. Dirisha hilo la usajili litafunguliwa rasmi tarehe 1 Julai 2022, na litafungwa tarehe 31 Agosti 2022.

Katika kipindi hicho pekee vilabu vyote vinatakiwa kukamilisha usajili wa wachezaji wote kwa wakati, pamoja na uhamisho wa wachezaji wa kimataifa. Vilabuvyote vinapaswa kuzingatia muda huo wa usajili ulioidhinishwa sababu hakuta na muda wa ziada baada ya dirisha hilo la usajili kufungwa.

Pia shirikisho hilo la soka Tanzania limesisitiza kwamba klabu yoyote atakayekutana na changamoto awasiliane na idara ya mawasiliano ya TFF. Aidha taarifa hiyo pia imeeleza kuhusu dirisha dogo la usajili kwamba litafunguliwa tarehe 16 Desemba 2022, na litafungwa tarehe 15 Januari 2023.
 
Kila la heri Wananchi katika kuimarisha kikosi chenu kwa ajili ya kutetea ubingwa wenu msimu ujao, na pia kwa ajili ya mechi za kimataifa.
 
Back
Top Bottom