SoC02 Disability is not inability

SoC02 Disability is not inability

Stories of Change - 2022 Competition

A man with one idea

Senior Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
126
Reaction score
268
MAZUNGUMZO NA YANGU KIPOFU MWENYE PhD.

Utangulizi,
Toka nilipoanza shule nilipitia mikono ya waalimu wengi sana. Shule ya msingi tu nilifundishwa na waalimu wasiopungua 18, sekondari nilifundishwa na waalimu wasiopungua 20 na kidato cha tano na sita nilifundishwa na waalimu wasiopungua 16. Chuo kikuu nilikutana na walalimu darasan na kwenye semina wasio pungua 40 hivyo waalimu ni rafiki zangu.

Nilifundishwa na waalimu wenye vyeti, diploma, degree, masters, PhD na Hata Maprofesa. Hivyo kwa kipindi nilichokuwa shulen kwa takriban miaka 18 nilipata uzoefu mkubwa wa kuwafahamu waalimu ndani nnje. Nakiri mchango wa waalimu ni mhimu sana katika Taifa. Watu wanaobeza waalimu, upeo wao ni mdogo sana.

Waalimu ndio chanzo cha proffesional zingine. Hakuna binadamu ambaye hajapitia mikono ya waalimu. Ukimuona Rais, Daktar, Mhandishi, Rubani wote wamepitia mikononi mwa waalimu. Waalim MUNGU AWABARIKI SANA.

KIINI.
waalimu wangu wengi walinigusa kwa namna mbalimbali, wengi wanafaa kuwa mfano wa kuingwa kwa kweli. Waalimu ni watu wenye siha njema.

Lakin Nilipokuwa chuo kikuu nilikutana na mwalimu mmoja(mhadhiri) ambaye alikuwa kipofu.

Mwalimu huyu alikuwa na Bongo kali sana na siha njema. alikuwa na sauti ikirindima hapo inavutia kuisikiliza. [Ikiwa wewe una mtoto mwenye ulemavu haimaaishi hana akili] usimfungie ndani.

Huyu mwalimu alikuwa anakuja kwenye mhadhara(darasani) bila kitu akiwa anatoa vitu kichwani. Nilishangaa najaza daftari kwa kufundishwa na mtu asiyeona. Niliona ana uwezo wa ajabu kwa kweli, alikuwa anachekesha atari, anadadavua vitu kwa kina, alikuwa anaeleweka sana. Kwa kweli fundisha yake niliipenda. Duuh nilipata A kwa kufundishwa na kipofu.

Siku moja niliamua kwenda kuzungumza nae ofcn kwake. Nilienda nikanunua shati nzuri sana nikaenda nalo ofcni kwake.

Nilibisha hodi nikaruhusiwa kuingia, alinipokea kwa furaha huku akinitazama machoni kama ananiona vile.

Nilimsalimia kimombo, akajibu kimombo kilichochanganyika na kifaransa, nilijibu kimombo na neno moja tu la kifaransa kwani sina ubebevu wa kifaransa. tuliangua kichecho kilichovuka dirisha.

Alifurah sana na kunikaribisha.nilimuomna radhi kufika oficn bila miadi, akaniambia relax my comrade karibu tuongee.

Office yake ilikuwa na mitambo mingi sana, ilikuwa nzuri kwa kweli nilivutiwa kukaa pale.

Nilikua mtu anayejiamini sana,niliweza kuongea na mtu yoyote huye haijalishi ni nani,hivyo sikuona shida kuongea nae.

Nilijitambulisha

Mimi John, baada tu ya kutaja jina langu aliniambia nilisoma Norway na rafiki anayeitwa Wisley Rebman. tukaendelea.

Nilimpa hongera kwa kazi njema anayoifanya.

Aliniambia hivi

Nukuu" comrade, mimi najikubali sana,ulemavu wangu haumaanishi uwezo mdogo, niliamua kujikubali na nikaenda shule kwa mazingira yaliyokuwa mavuri, nilisoma nikamaliza elimi ya _msingi,sekondar,advance,chuo kikuu nikachukua degree ta pili na PhD wakati sijawahi kuiona sura ya Dunia"

Nilijikuta naumia kwa kweli!


Aliendelea kusema

Nukuu
_Comrade Wisley, wewe una macho yanayoona,masikio,mikono,miguu unatumiaje viungo hivyo alivyokupa MUNGU?
"[emoji871]Je unatumia miguu yako kwenda wap?
[emoji871]Unatumia mikono yako kushika nini?
[emoji871]Unatumia macho yako kusoma nini?kutazama nini?
[emoji871]Unatumia masimio yako kusikiliza nini?"_
[Unatumia viungo vyako vya mwili kufanya nini, unajua kuna viungo unavyo wengine hatuna na sio kwa mapenzi yetu?]
Mwisho alisema " _natamani ningaliiona Dunia ilivyo,ningefanya mambo makubwa sana"

Nguli wa Elimu yule kwa kweli alinigusa sana.

Alinishauri akisema,viungo alivyokupa Mungu ni utajiri mkubwa sana. Ukivitumia vizuri utatajirika, utaisaidia familia yako,jamii, Taifa na Hata ulimwengu.

Kuanzia hapo nilijiona wa pekee sana, kimoyo moyo jilimshukuru Mungu kunipa viungo vyote vya mwili,

Ndani ya office ile nilifanya maamuzi kuwa, nitatumia viungo vya mwili alivyonipatia mwili kujisaidia mwenyewe, kuleta mchango kwa jamii na Taifa.

Nilimuiza maswali mengi ya maisha yake ya shule alinisimulia mambo mengi, Alinisimulia maisha ya Ulaya yalivyo mazuri alivyokuwa huko japo anasema "niliyahisi tu kwani sina macho"

Siku ile nilichota hekima nyingi sana toka kwa mzee yule ambazo hadi leo nazitumia maishani. Uishi sana Daktari,acha kisa hiki kiwe fundisho kwa wengine.

Nilitoa shati yangu iliyokuwa na tai yake nikamzawadia.

Nikamwambia
Nukuu"hii ni shati mwalimu,nimekupa zawadi,alifurah sana na kunishika mkono akautikisa vizuri, akaniambia nimekuwa hapa chuoni miaka mingi,lakin hakuna mwanachuo aliyewah kunipa zawadi, asante sana kijana wangu. Aliniombe heri maishani

Mwisho alinipa simu karatasi nikaandima namba yangu ya simu naye akanitajia yake nikaenda zangu kwangu.

Kesho yake alinipigia simu nikaenda ofcn, nilifika amevaa ile shati, akasema
Nukuu
"Wisley, Hii shati nilienda nayo kwangu, nikainajaribisha, mke wangu akaniambia umepenzeza sana, nikaamua niivae leo japo mimi siioni ala naamini nimependeza.
Tuishie hapa kwani naumia for sure.

Fundisho
●Ulemavu haimaanishi huna uwezo. KILA MTU ANA KITU CHA PEKEE NDANI YAKE
●Je wewe uliyena viungo vyote, UNAVITUMIAJE? tubadilike jaman
●Tuwapende watu wa aina zote. "Ongea na watu vizuri"

Kijana ni siha njema
Kijana ni bongo kali
Kijana ni mtazamo bulbul

John .
 
Upvote 0
Back
Top Bottom