P h a r a o h
JF-Expert Member
- Mar 25, 2024
- 785
- 1,413
- Thread starter
-
- #21
View attachment 3257477
Itakuaje Duniani Ambapo Kuzeeka itakua Hiari ?
Wataalamu wanasema AI na nanoboti zitaifanya ndoto hii kuwa halisi hivi karibuni.
( nanoboti, nanobot ni robot ndogo sana zisizoonekana kwa macho ya kawaida yaani roboti ndogo kama bakteria )
Mtabiri maarufu wa teknolojia, Ray Kurzweil, anadai kwamba binadamu wanaweza kufikia imortality ndani ya miaka mitano tu.
Kwa mujibu wa Kurzweil, maendeleo katika genetiki, nanoteknolojia, na akili bandia (AI) yatafanya iwezekane kuzuia mchakato wa uzeekaji wa mwili na hata ku upload fahamu za binadamu kwenye mfumo wa kidijitali.
Sehemu muhimu ya wazo hili ni nanoboti—roboti ndogo sana zinazoweza kutengeneza mwili wa binadamu kwa ngazi ya seli, hivyo kumfanya mtu kuwa na kinga dhidi ya magonjwa na uzee. Kurzweil anasema kuwa kadri teknolojia ya matibabu inavyoendelea, hatimaye tutaweza kuongeza umri wa maisha bila kikomo, na hivyo kifo kitakuwa hiari.
Ingawa wazo hili linaweza kuonekana kama sayansi ya kubuni, Kurzweil amekuwa mwenye maono sahihi mara nyingi, ikiwa ni pamoja na utabiri wa kukua kwa mtandao wa intaneti na ubora wa AI dhidi ya binadamu kwenye mchezo wa chess. Pia, anatabiri kuwa kufikia mwaka 2045, akili bandia itazidi uwezo wa binadamu, tukio linalojulikana kama "singularity".
Ingawa wengi wana hofia, maendeleo katika AI na bioteknolojia—kama kipandikizi cha ubongo cha Neuralink cha Elon Musk—yanaonesha kuwa binadamu wapo ukingoni mwa mapinduzi makubwa ya kiteknolojia.
Je, imortality ( kuishi milele ) itakuwa halisi kabla ya 2030? Bado haijathibitishwa, lakini utabiri wa Kurzweil unaendelea kuibua mijadala mikali kuhusu mustakabali wa maisha ya binadamu na AI.
Soma zaidi hapa:
[Ray Kurzweil says We’ll Reach IMMORTALITY by 2030 | The Singularity IS NEAR – Lifeboat News: The Blog
Msongo mkubwa wa mawazo ni hatari kwa Afya Yako ya mwili kuliko unavyodhani hizi ni sababu na jinsi ya kujikinga
Kuwaza sana mambo usiyoweza kudhibiti kuna madhara makubwa kwa afya yako ya mwili.
Msongo wa mawazo wa muda mrefu huweka mfumo wa mwili muda wote katika tahadhari ya kukabiliana na msongo hali hii ya tahadhari kila wakati, husababisha msongo sugu wa mawazo. Kadri muda unavyopita, hali hii hudhoofisha mfumo wa kinga, na hivyo kufanya mwili uwe rahisi kushambuliwa na magonjwa.
Zaidi ya hayo, msongo wa mawazo wa muda mrefu umehusishwa na matatizo ya moyo na mishipa ya damu, ikiwa ni pamoja na shinikizo la damu na hatari kubwa ya ugonjwa wa moyo.
Viwango vya juu vya homoni za msongo kama cortisol vinaweza pia kusababisha tatizo la mmeng'enyo wa chakula, mvutano wa misuli, na maumivu ya kichwa.
Zaidi ya hayo, mzigo wa kiakili wa kuhangaikia mambo yasiyoweza kudhibitiwa unaweza kusababisha tabia hatarishi, kama vile kula kupita kiasi au matumizi mabaya ya vilevi, hali inayoweza kuharibu zaidi afya ya mwili.
Soma zaidi:
[https://www.apa.org/topics/stress/body](https://www.apa.org/topics/stress/body)
Pata msaada:
[https://www.nimh.nih.gov/health/find-help](https://www.nimh.nih.gov/health/find-help)