P h a r a o h
JF-Expert Member
- Mar 25, 2024
- 785
- 1,413
- Thread starter
-
- #41
Je, ungelipa $200,000 ili uishi tena miaka ijayo baada ya kufa
Sasa unaweza. Maabara mpya ya cryonics inahifadhi miili kwa matumaini ya kufufuliwa siku moja wakati sayansi itakapokuwa imeendelea vya kutosha.
Tomorrow.Bio, maabara ya kwanza ya cryonics barani Ulaya, inalenga kuhifadhi miili katika joto la chini kabisa kwa matumaini ya kufufuliwa pale sayansi ya matibabu itakapoweza kutibu magonjwa yaliyosababisha vifo vyao.
Licha ya wasiwasi wa wanasayansi na ukosefu wa mafanikio ya kufufua mtu yeyote hadi sasa, kampuni hiyo tayari imehifadhi miili ya wateja wachache na wanyama vipenzi, huku wengine 700 wakiwa wamejiandikisha. Utaratibu huu unahusisha kubadilisha maji ya mwili na kemikali maalum zinazozuia uharibifu wa seli kwa barafu, kisha kupooza mwili hadi -196°C na kuuhifadhi kwa muda usiojulikana.
Mwanzilishi wa Tomorrow.Bio, Emil Kendziorra, anafananisha wazo hili na maendeleo mengine ya kitabibu kama upandikizaji wa viungo, ambao hapo awali ulionekana kuwa haiwezekani.
Wakosoaji wanasema cryonics inakabiliwa na changamoto za kimaadili, kisayansi, na kivitendo. kuharibika kwa mwili huanza mara tu maisha yanapokoma, na hata kama kufufuka kutakuwa kunawezekana, hakuna uhakika kama muundo wa neva wa ubongo—ambao ni msingi wa kumbukumbu na utambulisho—utaweza kurejeshwa.
Hata hivyo, wafuasi wake wanaiona cryonics kama dau lenye thamani ya kuwekwa. Baadhi ya wateja wake, wanaogharimia uhifadhi wao kupitia bima ya maisha, wanaiona kama aina ya usafiri wa muda ( Time Travel ), wakikumbatia wazo la kupata fursa ya pili ya kuishi. Tomorrow.Bio ina malengo makubwa, ikiwa ni pamoja na kuhifadhi muundo wa neva mwaka huu 2025 na kufanikisha uhifadhi unaoweza kurejeshwa ifikapo 2028.
Ingawa cryonics bado ni sayansi inayobishaniwa, umaarufu wake unaonyesha tamaa ya binadamu ya kurefusha maisha—na labda siku moja, kukishinda kifo.
Soma zaidi: Home - Tomorrow Bio