Dismas Massawe, Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi-ETDCO: Miundombinu duni vijijini inachangia baadhi ya Miradi kutokamilika kwa wakati

Dismas Massawe, Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi-ETDCO: Miundombinu duni vijijini inachangia baadhi ya Miradi kutokamilika kwa wakati

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
IMG_4654.jpeg

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba ametoa wito kwa Kampuni ya ETDCO ambayo ni kampuni tanzu ya Tanesco kuongeza ubunifu zaidi katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo kutumia vifaa vyenye teknolojia bora vinavyoenda na Dunia ya sasa.

"ETDCO mnaendelea vyema na jitihada za utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya umeme, igieni kwenye Dunia ya ubunifu na kutumia vifaa vyenye teknolojia sahihi kwa nyakati hizi" amesema Katibu huyo

Ameyasema hayo Julai 9, 2024 kwenye maonesho ya 48 Kimataifa ya sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa matumizi ya teknolojia bora yataongeza tija kwenye ufanisi wa miradi wanayoitekeleza.

Aidha kwa Dismas Massawe ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za ufundi wa ETDCO, ambayo ni kampuni tanzu ya shirika la umeme Tanzania (Tanesco ) inayofanya kazi za ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme, amesema kuwa kampuni hiyo unatekeleza miradi mbalimbali nchini, ikiwemo eneo la Msomera mkoani Tanga.

"Tuna mradi wa Msomera ambao ni wa kujenga miundombinu ya usambazaji wa umeme katika nyumba 5,000 zilizojengwa na Serikali, na mpaka sasa tunasambaza umeme kwenye nyumba 2500 za awali"

IMG_4612.jpeg

Ameongeza kuwa mradi kupeleka umeme eneo hilo la Msomera una thamani ya Bilioni 33. Pia ameeleza kuwa baada ya Serikali kukamilisha ujenzi eneo la Simanjiro na Kilindi kwa ajili ya wakazi wanaotarajiwa kuhamia maeneo hayo nako watahusika kwenye mchakato wa kufikisha umeme kwenye makazi hayo kabla ya mwaka huu kukamilika.

Lakini amedai kuwa wamekuwa wakikumbana na changamoto kwenye baadhi ya maeneo kutokana na miundombinu duni ya barabara ambayo wakati mwingine uwafanya washindwe kukamilisha miradi kwa wakati au kutumia gharama zaidi katika kufikisha baadhi ya vifaa kwenye maeneo ilipo miundombinu.

"Maeneo mengi tunayopeleka vijijini ni maeneo mapya miundombinu ya kufikisha 'material' mara nyingi inakuwa ni ngumu sana sehemu nyingine hazina barabara tunalazimika kutumia namna mbalimbali za kupeleka umeme katika maeneo hayo"amesema Massawe

Ameongeza kuwa licha ya jitihada mbalimbali ambazo wamekuwa wakizifanya lakini changamoto nyingine ambayo imekuwa kikwazo kwao baadhi ya vipindi ni mvua kubwa zilizonyesha na kuaribu baadhi ya miundombinu ya barabara hali ilichangia baadhi ya miradi kutokakamilika kwa wakati.
 
Back
Top Bottom