Skewed sio tatizo, tatizo ni pale ratio inapokuwa mbaya kiasi hicho, angalia vizuri hiyo video. Mmarekani wa kawaida inabidi afanye kazi mwaka mzima kupata pato la saa moja la CEO. Hii ni mbaya sana. Kuna model za mifano kama vile Norway, sweeden, Finland etc, huko distribution ipo poa na kila mtu ana furaha na uchumi wa nchi. Huko Marekani kuna mfumo mbaya zaidi wa afya, yaani kuna watu hawana uhakika wa kupata matibabu punde anapougua. Pia maskini wa kutupwa wapo, watu wa aina hiyo huwezi kuwakuta Finland kwa mfano
Mimi sio mchumi, ila ubepari wa aina hiyo nahisi ni hatari, napenda economic model za nchi za scandinavian. Au unasemaje Kiranga?