DIT inaongoza kwa kufelisha wanafunzi? Tatizo ni nini hasa? Nini kifanyike?

Sababu ya kufeli mie kusema ukweli siwezi kuijua. Mitihani sijaiona, wala wanafunzi sijaongea nao.

Ila ninachoweza kuongeza kwenye hii mada ni kushare na nyiniyi experience kutoka kwa ndugu wangu anayesoma huko. Yeye ansoma I.T. Kwahiyo fikiria masomo ya programming , networking etc... Sasa alinidokeza mwezi wa Saba kwamba kule chuoni hawana internet mwezi wa nne sasa. ! Nikammuliza sasa hizo assignment mnafanya research kivipi akaniambia kupitia material ya waliopita.

Sasa likaja swali la programming. Wao wanaruhusiwa kutumia computer (kumbuka hazina internet) masaa machache kwa wiki tuu- siku nyingine hawawezi kwasababu wanafunzi wamejaa. Programming wanakaa darasani wanamsikiliza mwalimu anavyoandika ubaoni !.... Nikasema Mungu wangu unajifunza programming kwa kutumia ubao , akasema ukitaka msaada kutoka kwa wanafunzi wanaoelewa (akili zinazo chaji) wanakuambia leta hela kwanza ndio nitakuelekeza.

Sijasema hili ndilo tatizo ... kuna idara nyingine pia engineering n.k...nao wamefeli. Lakini ni mchango wangu labda utasaidia kupanua mawazo kidogo

B.P (2010)
 
tatizo la pande zote..ukosefu wa walimu na vifaa vya kufundishia vya kisasa na wanafunzi pia
 
...Sasa alinidokeza mwezi wa Saba kwamba kule chuoni hawana internet mwezi wa nne sasa...
*Hili inawezekana kuwa ni tatizo!

Nikammuliza sasa hizo assignment mnafanya research kivipi akaniambia kupitia material ya waliopita.
*yaani hapa kama waliopita walikosea hizo programming, pia hawa wadogo zao nao wata kopi matango, mmmh!

Sasa likaja swali la programming. Wao wanaruhusiwa kutumia computer (kumbuka hazina internet) masaa machache kwa wiki tuu- siku nyingine hawawezi kwasababu wanafunzi wamejaa.
*hii inamaanisha ni uhaba wa vitendea kazi

Programming wanakaa darasani wanamsikiliza mwalimu anavyoandika ubaoni !.... Nikasema Mungu wangu unajifunza programming kwa kutumia ubao
*hili ni tatizo kubwa sana.....wanahitaji mabadiliko makubwa sana!

akasema ukitaka msaada kutoka kwa wanafunzi wanaoelewa (akili zinazo chaji) wanakuambia leta hela kwanza ndio nitakuelekeza.
*hii tunasema kufa kufaana! je kama mtu hana hela? ndo imekula kwako lol!

***Sijui serikali ya DIT kama imeshawahi kukaa na kutafakari juu ya hili suala!
 

Tatizo ni mifumo mibovu kwa ujumla katika nchi yetu isiyozingatia vipau mbele, tunamifumo inayotukuza siasa na si maendeleo ya nchi. Haingii akilini mtu afundishwe kitu kama programming ubaoni!, tunahitaji kiongozi atakaye badili mwelekeo wa nchi yetu, watanzania tuamke.
 
Hivi mkuu wa hiki chuo bado ni yule Profesa kilaza Kondoro? Kama bado ni yeye, wala sishangai hali hii kutokea.
 
Hivi mkuu wa hiki chuo bado ni yule Profesa kilaza Kondoro? Kama bado ni yeye, wala sishangai hali hii kutokea.

Prof. J.W.A. Kondoro - Principal, Dar es Salaam Institute of Technology
Kwanini unamwita Kilaza? Tupe data tafadhari!
 
Kwanini unamwita Kilaza? Tupe data tafadhari!
Tangu awe principal wa chuo kile haya ndiyo yanayoendelea katika chuo chake...

Mambo mengi yako ndani ya uwezo wake kuyakabili. Kama si ukilaza ni kitu gani? Unajua kusoma sana si kuelimika!!
 
Tangu awe principal wa chuo kile haya ndiyo yanayoendelea katika chuo chake...

Mambo mengi yako ndani ya uwezo wake kuyakabili. Kama si ukilaza ni kitu gani? Unajua kusoma sana si kuelimika!!
mmmmh, nimekusoma! nadhani safari hii atalifanyia kazi! mi nadhani wao wanafurahia kuona wanafunzi wakipata 'supl', 'disco'...sijui hawajiulizi tatizo ni nini? Kwani hawana evaluation kwa wakufunzi wa wanafunzi?:confused2:
 
Mambo mengi yako ndani ya uwezo wake kuyakabili. Kama si ukilaza ni kitu gani? Unajua kusoma sana si kuelimika!!
Sidhani kama ana uwezo huo, yeye ni Prof wa Physics, sasa unatarajia nini? Nadhani ni wakati wa kufanya mabadiliko makubwa, hastahili kuendelea kukaa hapo!
 

Hapo penye nyekundu, pananishitua. Kama waliofeli wanazidi watahiniwa basi wanachuo WOTE wamefeli.

Kuhusu wanafunzi kutokufanya vizuri mitihani yao ni suala mtambuka.

Ili kulijadili vizuri na kupata ufumbuzi inabidi uanzie kwenye selection criteria zinazotumika, ufundiishwaji, uelewa wa wanafunzi, ushiriki wa wanafunzi katika seminars,home works, group works, practicals na field works.

Upande wapili uangaliwe mtaala wanaotumia,uwepo wa vifaa vya kufundishia na kwa wafundishaji na wafundishwaji, utungwaji wa mitihani, usahihishaji na utoaji wa majibu(yaani vigezo nani kafaulu na nani kafeli).
 
Sidhani kama ana uwezo huo, yeye ni Prof wa Physics, sasa unatarajia nini? Nadhani ni wakati wa kufanya mabadiliko makubwa, hastahili kuendelea kukaa hapo!
Unamaanisha kwamba mtu anayestahili kukaa katika nafasi hiyo ni lazima awe amesomea mambo ya 'management'??
 
Hapo penye nyekundu, pananishitua. Kama waliofeli wanazidi watahiniwa basi wanachuo WOTE wamefeli.
Samahani, nilimaanisha 'uwiano wa wanafunzi waliofeli na idadi ya waliotahiniwa'

Kuhusu wanafunzi kutokufanya vizuri mitihani yao ni suala mtambuka. .
hapo kwenye red tafadhari, hii inamaanisha nini?
 

Tatizo namba moja la DIT ni kuondoka kwa Dr. Richard Masika.

Tatizo namba mbili ni kuwepo kwa mhadhiri mmoja mfupiii (jina tunalo). Hajui na hajui kama hajui.



Tatizo la Tatu ni ubia wao na vyuo vya Uchina. (Nafikiri kila mtu anafahamu namna wachina walivyogeuza nchi yetu dampo la vitu vya hovyo hovyo. Walimu wengi wa DIT wanaenda kupigwa msasa China. Kwa hiyo usitegemee kuna walimu wazuri DIT. Sahau.

Mwisho ni mazingira. Ni katikati ya jiji. Kwa hiyo kuna vurugu na vishawishi vingi. Mfano, pembeni kidogo kuna sehemu inaitwa Mabatini, maarufu kwa machangudoa wa ''Buku''. Mbele kidogo, kuna mahali barabara ya Uhuru inakutana na Lumumba, maarufu kwa machangudoa wa bei mbaya. Mbele kabisa kuna Ohio, huko kila mtu anafahamu kuna nini. Mbele zaidi kuna Joly Club, huko ni baraa (hata mashoga utawakuta). Kati kuna Bills (kila Alhamisi ni Ladies Free).

Kama hayo yote hayajaonekana kuwa tatizo kwa uongozi, na kuchukuliwa hatua, basi yana mkono wake katika matokeo mabovu unayosema.
 
kuna kipindi ilisemekana degree zao hazilkidhi viwango compared na za Udsm, nahisi wanataka wenyewe wajulikane kwamba ni wagumu pia (nimawazo yangu). kuna mfanyakazi mwenzangu yuko pale electrical anaingia 3rd yr wanapata tabu kweli esp wale wa evining ambao wanajulika ni wafanyakazi na wanaingia na magari pale, full kukomolewa
 
Tatizo namba moja la DIT ni kuondoka kwa Dr. Richard Masika.
**Poor him

Tatizo namba mbili ni kuwepo kwa mhadhiri mmoja mfupiii (jina tunalo). Hajui na hajui kama hajui
.
**Oh, its so sad if he is not aware of his problem!

Tatizo la Tatu ni ubia wao na vyuo vya Uchina. (Nafikiri kila mtu anafahamu namna wachina walivyogeuza nchi yetu dampo la vitu vya hovyo hovyo. Walimu wengi wa DIT wanaenda kupigwa msasa China. Kwa hiyo usitegemee kuna walimu wazuri DIT. Sahau.
**I've been asking myself, why most of DIT staffs go for their PG education in China? I see!

**Hili linaweza kukwepeka kwa uwezo wa mwanafunzi binafsi! Kama mtu umeenda shule ana unania ya masomo, hili siyo tatizo! Ninauhakika hata wanafunzi wa UDSM nao huenda hizo ladies free!

Kama hayo yote hayajaonekana kuwa tatizo kwa uongozi, na kuchukuliwa hatua, basi yana mkono wake katika matokeo mabovu unayosema.
**I am comfident this time something good will come up. Lets hope for the bes.
 

mimi ni mhitimu wa DIT mwaka mmoja uliopita BEng Civil,matatizo ya DIT ni ya pande zote mbili wakufunzi pamoja na wanafunzi.
 

Matatizo ya DIT hayajaanza leo wala jana, ni suala la muda mrefu sana. Wala kuondoka kwa Dr. Masika sio sababu ya hizo failures. Nitakupa mfano hai, wahitimu wa telecom (ADE01T) wa mwaka 2004, takriban 90% walikuwa wamefeli projects zao (wakati huo wakitahiniwa na NECTA). Baada ya kujitokeza kwa hali hiyo na DITSO kufuatilia kwa makini kwa uongozi wa chuo na NECTA, matokeo yalibadilishwa ghafla na walioonekana kufeli project walikuwa kama 5%. Kwahiyo mfumo mzima wa uendeshaji wa chuo ni mbovu, hapa ninamaanisha management ya DIT ni mbovu sana na kwa sehemu kubwa imechangiwa na huyo mtaalamu wa nuclear, ni mbishi, anajifanya much know, nadhani kwa kuwa yeye pekee ndiye Profesa hapo chuoni basi anaamini kwamba anaweza kufikiria kwa niaba ya wengine.

Sababu nyingine ya msingi sana ni uchakavu wa miundombinu,i.e madarasa, karakana, maabara na vifaa vya kujifunzia na kufundishia, hata ofisi za wahadhiri ni tabu tupu, wanabanana kwenye "vi-cube" utadhani wanafunzi wa sekondari bana.

Na huo ubia na wachina nao ndio unazidi kushusha hadhi ya taaluma hapo DIT, pamoja na kuteua wakuu wa idara kwa kuangalia nani ni "yes sir". Utashangaa mkuu wa idara hana quality yoyote ya kumfanya awe na nafasi hiyo lakini ndiye mkuu wa idara.

Kwa ujumla Kondoro amefikia mwisho wa upeo wake wa uongozi, hadi hapo atakapostafu au kuondolewa hapo dit, vinginevyo tutarajie ubora wa elimu kuzidi kudorora.
 
mimi ni mhitimu wa DIT mwaka mmoja uliopita BEng Civil,matatizo ya DIT ni ya pande zote mbili wakufunzi pamoja na wanafunzi.
Unaweza kutupa 'data in detail' ni matatizo gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…