son of a teacher
JF-Expert Member
- Jul 30, 2017
- 541
- 1,449
Kwa wapenzi wa Mchiriku/Mnanda jina la Division Haji litakuwa sio geni sana haswa kwa ukanda wa Temeke, ni mpiga ngoma hodari hakika ukihudhuria show zake lazima uburudike na ufurahi kwa ufundi na ustadi uliotukuka kwa namna anavyopiga ngoma.
Alikuwa mpiga ngoma wa Omary Omary "Atomic", kisha akawa mpiga ngoma wa Juma Mpogo "Seven Survivor", na baada ya Mpogo kufariki na bendi ya Seven kusuasua na kuzaa bendi zingine saizi anatumika kupiga ngoma kwenye makundi karibia matatu au manne.
Atomic wanamtumia, Miami Voice wanamtumia, Seven na hata kundi jipya la Dogo Kiedu wanamtumia. Makundi yote yanamtumia kwa namna alivyo na uwezo wa kipekee.