Division Haji: Fundi wa kupiga ngoma wilaya ya Temeke

son of a teacher

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2017
Posts
541
Reaction score
1,449
Kwa wapenzi wa Mchiriku/Mnanda jina la Division Haji litakuwa sio geni sana haswa kwa ukanda wa Temeke, ni mpiga ngoma hodari hakika ukihudhuria show zake lazima uburudike na ufurahi kwa ufundi na ustadi uliotukuka kwa namna anavyopiga ngoma.

Alikuwa mpiga ngoma wa Omary Omary "Atomic", kisha akawa mpiga ngoma wa Juma Mpogo "Seven Survivor", na baada ya Mpogo kufariki na bendi ya Seven kusuasua na kuzaa bendi zingine saizi anatumika kupiga ngoma kwenye makundi karibia matatu au manne.

Atomic wanamtumia, Miami Voice wanamtumia, Seven na hata kundi jipya la Dogo Kiedu wanamtumia. Makundi yote yanamtumia kwa namna alivyo na uwezo wa kipekee.

Attachments

  • IMG_20221214_143111.jpg
    88.3 KB · Views: 10
Safi sana mtoa mada,uzi mzuri sana.Umetumia vizuri jukwaa kumulika sehemu ambazo mwanga umekuwa adimu kupenya.Kupitia wewe nimemjua mtu mwenye kipaji kizuri kisichopewa nafasi ya kutosha kwa hadhira iliyotawaliwa na usasa.
 
Kabisa ndugu..Hadi nimeandika Uzi huu jamaa ni gwiji kwenye ngoma ,kipaji halisi

Jamii nyingine angekuwa mbali sababu ni kipaji Cha uhalisia wa kuchezea ngoma zaidi ya 2,3 bila mixing ya computer
 
Kabisa ndugu..Hadi nimeandika Uzi huu jamaa ni gwiji kwenye ngoma ,kipaji halisi

Jamii nyingine angekuwa mbali sababu ni kipaji Cha uhalisia wa kuchezea ngoma zaidi ya 2,3 bila mixing ya computer
Nimekulia kibaha mkoa wa pwani,naelewa kidogo kuhusu hayo mambo ya mdundiko na mchiriku,wengi hawatakuelewa humu.
 
Uvah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…