Diwani Haji Fundi Haji ahimiza usafi wa mazingira Kata ya Bondeni

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
256
Reaction score
259
Diwani wa Kata ya Bondeni Manispaa ya Moshi ,Haji Fundi Haji amewataka wananchi na wafanyabiashara wa Kata hiyo kuhamasishana na kushiriki kikamilifu katika suala zima la usafi wa mazingira na kuifanya kata hiyo kuwa moja ya Kata zinazoongoza kwa usafi.
Wito huo ameutoa wakati akizungumza na wananchi wa Kata hiyo kwenye kilele cha siku ya usafi wa mazingira katika hiyo.

Kata ya Bondeni ndiyo Kata pekee yenye masoko mawili makubwa ya nafaka ambayo ni Mbuyuni na Manyema hivyo suala la usafi wa mazingira ni Moja ya vipaumbele muhimu kwa wananchi na wafanyabiashara katika Kata hiyo kutokana na kupokea watu wengi Kila siku .

Hapa chini tunakuletea picha mbali mbali wakati wa zoezi la usafi wa mazingira Kata ya Bondeni likiongozwa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Nurdin Babu
 

Attachments

  • IMG_5976.jpg
    1.1 MB · Views: 13
  • IMG_5897.jpg
    1.2 MB · Views: 13
  • IMG_5895.jpg
    1.2 MB · Views: 12
  • IMG_6007.jpg
    987.1 KB · Views: 12
  • IMG_6017.jpg
    1.1 MB · Views: 13
  • IMG_6008.jpg
    1 MB · Views: 9
  • IMG_5943.jpg
    1.4 MB · Views: 13
  • IMG_5890.jpg
    1.3 MB · Views: 11
  • IMG_5942.jpg
    1.4 MB · Views: 10
  • IMG_6016.jpg
    1.1 MB · Views: 13
  • IMG-20260920-WA0055.jpg
    226.4 KB · Views: 13
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…