A
Anonymous
Guest
DIWANI KATA BAKOBA ANALAZIMISHA KUBADILISHA MATUMIZI YA FEDHA UJENZI WA SOKO LA DAGAA.
Diwani wa kata ya Bakoba Manispaa ya Bukoba Ndg, Shaban analazimisha kuhamishwa kwa fedha Tsh Mil 28 zilizotolewa na Waziri Mkuu kwa ajii ya kuanza ujenzi wa soko la dagaa kwenda kwenye ujenzi wa Zahanati katika eneo la Nyakanyasi kinyume cha utartibu.
Diwani huyo anashirikiana na watia saini wawili kwenye kata hiyo ili kufanikisha jambo hilo.
Kwa mujibu wa mjumbe wa baraza la kata ni kwamba hivi karibu Mkurugenzi wa mnispaa ya Bukoba aliziazima fedha hizo bila wao kujulishwa na tayari amerejesha shilingi milioni 4.
Mjumbe huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema fedha hizo zipo kwenye akaunti ya kata kwa zaidi ya miaka minne licha ya Mamlaka ya Bandari kuwachangia trip mbili za kokoto,Trip mbili za mchanga na Trip mbili za mawe.
Anasema nchakato wa kubadilisha matumizi ya fedha hiyo ni dhairi shairi lengo ni kuzitafuna kwa kushirikiana na wajumbe baadhi na viongozi.
Hata hivyo mjumbe huyo anasema Mkurugenzi wa Manispaa alishapewa taarifa ya mkwamo wa fedha hizo lakini alikataa kujiingiza kwenye mvutano na diwani.
Mji wa Bukoba licha ya kuwa umepakana na ziwa Victoria bado hauna soko maalumu la samaki na dagaa kama ilivyo miji mingine iliyopakana na Ziwa Victoria hali inayosababisha samaki kuuzwa mahala popote huku serikali ikikosa mapato.