Diwani Moshi matatani, TRA yafunga akaunti zake

Diwani Moshi matatani, TRA yafunga akaunti zake

Fred Mwakitundu

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
227
Reaction score
382
Taarifa kutoka Moshi zinatonya kuwa diwani mmoja wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Manispaa ya Moshi ameingia matatani baada ya kubainika amekuwa akiendesha biashara ya utoaji wa mikopo bila kuwa na leseni na hivyo kukwepa kodi .

Kwa sasa Diwani huyo(jina kapuni)anachunguzwa na TRA kwa ukwepaji wa kodi na utakatishaji wa fedha na kwa mujibu wa taarifa hizo Mamlaka hiyo ya mapato imefunga akaunti zake.

Diwani huyo ambaye kabla ya hapo alikuwa kada wa CHADEMA,amekuwa akiendesha biashara ya kukopesha fedha watu na kuwatoza riba kubwa ya aslimia 20 lakini amekuwa na mchezo wa hovyo wa kupoka mali za watu pindi wanaposhindwa kurejesha mikopo hiyo hata kwa siku moja .

Mbaya zaidi ni kuwa,akikukopesha muda wa kurejesha ukikaribia anazima simu na kuondoka mjini lengo ni kuchukua dhamana ya mkopaji.

Unataka jina lake na kata anayotoka?

Kesho naweka hapa majina yake ili tumfahamu na msimamo wa chama chake kuhusu vitendo hivyo ambavyo vinamwondolea sifa ya kuendelea kuwa diwani
 
Kama ni mwanaCCM hiyo kwake nyepesi sana anamalizana nao mapema tu saa nne asubuhi.
 
Ndio kawaida ya MATAGA kula vya watu kwa lazima.
MATAGA ni janga zaidi ya Korona.
 
Ndo faida ya kujiunga na mashetani.... hamna kesi hapo mashetani wenzie watamwokoa
 
Back
Top Bottom