Diwani, toka uwaelezee wanaosema una miaka 10 hujawahi kusoma mapato na matumizi

Diwani, toka uwaelezee wanaosema una miaka 10 hujawahi kusoma mapato na matumizi

Joined
Jul 6, 2024
Posts
97
Reaction score
72
Nikaota ndotoni nikajikuta nasema:

Diwani,

Watu wanasema mengi juu yako. Eti wewe huna elimu ya kutosha kumudu uelewa wa mambo makubwa. Nakuomba, kwa kuheshimu katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo la 2005 ibara 08(1)(a)(b)(c)(d), na kwa kuzingatia ibara 26(1) na ibara 09 a, b, f, h, tokea hadharani upangue hoja.

Onyesha cheti. La saba ulisomea wapi? Ulidai sekondari umesoma mpaka fomu ya Kati. Ulisoma na nani, Diwani? Ulisoma masomo gani? Mwalimu gani wa shule hiyo unamkumbuka?

Kumbuka, Diwani, uliapa kuilinda, kuihifadhi, na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na usisahau ibara 35(1). Ikibainika ulidanganya, wananchi tunakusudia kukushitaki kwa kutoa taarifa za feki na za uongo kuhusu elimu yako.

Kumbuka, Diwani, Katiba ya CCM 1977 toleo 2022 ibara 08(2)(6), ibara 13(1) c,d,e, ibara 19(1) c,d, ibara 15(4) i(7)bara 12(1)(a) uk 152, ibara 01, 08, 09, Ilani ya CCM 2020 uk 01 ibara 04. Ujikumbushe ikiwa, Diwani, ulishitiki kutoa taarifa za uongo kuhusu elimu, ujue umeivunja Sheria the Political Parties Act Chapter 258 na umeivunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nakuomba sana, Diwani, tokeza hadharani, ukanushe. Wanaosema hujui kuandika, tokea hadharani uandike. Wanasema hujui kusoma, tokea hadharani usome walau gazeti la michezo. Wanaosema una miaka kama 10 hujawahi kusoma mapato na matumizi toka uwaelezee.

Nikashtuka katika Kongamano la Ulimwengu wa Kiroho huko ndotoni lililofanyika kata ya Nkiwanzeenza wilaya ya Ilyalyaha. Mukoha wa Ndolusalimyu.
 
Back
Top Bottom