Diwani wa CCM Iringa awaguza waliofeli kidato cha nne mtaji wa kisiasa

Joined
Feb 8, 2012
Posts
92
Reaction score
9
Diwani wa CCM ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu aja na mpango kabambe utakaorahisishia wahitimu wa kidato cha nne waliofeli mtihani wa Taifa 2012 kujiunga vyuo mbalimbali vikuu.

Katika mpango huo wahitimu wataanza kusoma kozi fupi fupi zenye vymasomo ya Hisabati, Kiingereza na Maarifa ya Jamii.

Baada ya kumaliza kozi hizo watasoma tena kwa kuunga unga mpaka wapate sifa za kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali bila ya kwenda kidato cha tano. Diwani huyo amekutana na wahitimu mbalimbali walioshindwa mtihani katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Ruaha na kuja na mikakati hiyo kabambe chini ya kauli mbiu ya ''TUMAINI JIPYA''. Mabweni ya Chuo Kikuu cha Ruaha kutumika kulaza wanafunzi hao wakati wa likizo.

Ina maana wale wote waliopata madaraja ya nne ya point za mwisho na sifuri watajumuishwa katika mpango huu.

Source : Tanzania Daima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…