Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Dude!.........Kwa hiyo Msando aligombea Udiwani kupitia CDM ili apate ulaji mbali na fani yake ya Uwakili!...........halafu ukiwa Diwani wa CDM hivyo wewe unawakilisha CDM tu..............hizo societies za huko Marekani (especially Tea Parties za GoP) zimekuathiri mazee...........
NyaniNgabu,
Siasa unayofanya wewe mimi sifanyi. Kwanza perception hazinilazimishi kufanya au kutokufanya uamuzi fulani. Endapo nitaruhusu 'wanachofikiri' watu kufanya maamuzi nitakuwa najikosea pamoja na jamii inayonizunguka.
Tuna tatizo. Wengi wanaangalia zaidi jamii inaona nini badala ya kufanya kile ambacho ni HAKI. Huo ni unafiki.
Rostam ana HAKI ya kutetewa. Msingi mmoja wa Katiba ni 'innocent until proven guilty'. Huwezi kuupinga msingi huo hata kama ni Rostam au Lowassa. Ingekuwa inawezekana basi wangekuwa jela.
Tusiwe na siasa za unafiki. Tusiogope kusimamia maamuzi ya HAKI kisa watu wataonaje.
Kuhusu uwakili na udiwani, vinaenda pamoja. Ukisema eti niache moja nibaki na moja unakosea. Kama itabidi tufanye hivyo basi wengi tutakuwa nje ya siasa....kuna msemo sikumbuki ni MwanaJF gani anautumia...'siasa isiachwe kwa watu fulani pekee...'
Husninyo,
Niseme hivi, Rajab Nkya sio fisadi. Naamini hivyo. Tuhuma dhidi yake ni za kisiasa kama zilivyo za Mh. Mbowe, Dr. Slaa, Lema na wengineo.
Sio kwamba sielewi mkanganyiko unaoweza kuwepo. Nililaumiwa sana kumfungulia kesi Mh. Grace na Lucy Owenya kutaka tafsiri ya mahakama kuhusu uhalali wa Mbune wa Viti Maalumu kuingia kwenye Halmashauri kisa tu anafanya kazi kwenye Halmashauri hiyo.
Atakayenihukumu kwa hilo anakosea. Jukumu langu kama wakili na diwani ni kutetea HAKI. Sio HAKI ya Chadema pekee, ni HAKI ya mtu yeyote anayestahili kutendewa HAKI. Maoni ya jumla yasituzuie kusimamia yale tunayoaamini.
Chadema kama kweli wapo makini wasiwape hawo mawakili nafasi za uongozi katika chama chao, wabakie kama wanachama wa kawaida, mimi naona kama mchezo wa kuigiza wanafanya Chadema wanazunguka nchi nzima wanafanya maandamano huku wanataja orodha ya MAFISADI, cha kuchekesha MAFISADI wakifishwa mahakamani hao hao viongozi wa Chadema mawakili wanachukuwa pesa za MAFISADI wanawatetea mahakamani kuwa hawa sio MAFISADI, hizi ndio siasa za Tanzania utapeli mtupu
cdm wachunge sana wananchi wasijesema hii kutaji orodha ya mafisadi ni
njia ya kuwatafutia wanasheria wao ulaji (tenda)
Husninyo,
Niseme hivi, Rajab Nkya sio fisadi. Naamini hivyo. Tuhuma dhidi yake ni za kisiasa kama zilivyo za Mh. Mbowe, Dr. Slaa, Lema na wengineo.
Sio kwamba sielewi mkanganyiko unaoweza kuwepo. Nililaumiwa sana kumfungulia kesi Mh. Grace na Lucy Owenya kutaka tafsiri ya mahakama kuhusu uhalali wa Mbune wa Viti Maalumu kuingia kwenye Halmashauri kisa tu anafanya kazi kwenye Halmashauri hiyo.
Atakayenihukumu kwa hilo anakosea. Jukumu langu kama wakili na diwani ni kutetea HAKI. Sio HAKI ya Chadema pekee, ni HAKI ya mtu yeyote anayestahili kutendewa HAKI. Maoni ya jumla yasituzuie kusimamia yale tunayoaamini.
Kusema niache uwakili na kubaki diwani inaonyesha hujui unachoongelea. Sifa mojawapo ya Diwani kwa mujibu wa sheria ni kuwa na kipato halali. Sasa nikiacha kuwa wakili kipato halali napata wapi? Hilo hulioni!
je kama mimi ni daktari na hao mafisadi wamekuja kwangu kwa ajili ya matibabu nifanyaje, nisiwatibu? is it not unethical,immoral and unproffesionalKwa hiyo mie kama ni mhandisi rostam akinipa kazi ya kihandisi nisifanye? Mie nitafanya sana