Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Diwani wa kata ya Buzuruga ambae pia ni naibu Meya wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela Manusura Sadick amefanyiwa dua maalum baada ya kutoka hospitali ya rufaa ya kanda ya Bugando alipokuwa anapatiwa matibabu ya majeraha aliyopata kutokana na kushambuliwa na kundi la vijana.
Diwani huyo alishambuliwa February 18 mwaka huu akiwa bar ya The Breeze wakati akitafuta chakula ndipo vijana hao wa itifaki walipotokea na kuanza kumshambulia hali iliyopeleka kupata maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mara baada ya kutoka hospitali ya Bugando alipokuwa anapiatiwa matibabu diwani huyo aliamua kufanya dua maalum ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kunususru Maisha yake
Imamu wa msikiti wa Nyambiti Sheikh Mohamed Almas amewataka wanachama wa CCM pamoja na wananchi kuishi kwa amani na kumlinda diwani huyo.