Diwani wa Kata ya Marangu Mashariki Jimbo la Vunjo, Jonas Mawala ameweka wazi kuwa ahadi nyingi walizo ahidi kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo hilo Dk.Charles Kimei wamezitekeleza na hakuna wanacho daiwa na Wananchi.
Ametoa kauli hiyo Aprili 17, 2025 wakati akielezea mafanikio yaliyopatikana katika kata hiyo ikiwemo ujenzi wa kituo kipya cha afya Marangu Headquarters kilichogharimu kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 500.
"Tumetimiza ahadi zote tulizo ziahidi na kwenda mbele zaidi vitu vingine ambavyo hatukuahidi vilijitokeza na tukavifanya, kwahiyo mimi ndio nawadai wananchi,wao hawanidai chochote nilipita kwenye vijiji nawauliza kama kuna kitu wananidai wanasema Mheshimiwa inatosha" Mawala.