Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Kampeni leo zimeanza rasmi za uchaguzi wa serikali za mitaa.
Ni muda wa kusikia tambo, majivuno, kejeli lakini na hoja nzuri na za hovyo. Leo tuanza na Kata ya Wazo moja ya mtaa na yakasikika maneno haya.
“Ndugu zangu siri ya ushindi wa Chama Cha Mapinduzi ni umoja miongoni mwa wanaCCM. WanaCCM tukiwa wamoja na tukatambua thamani ya Chama chetu na kwamba Chama hiki ndicho kimeshika Dola na amani ya Taifa letu la Tanzania...tukasimame kukipigania Chama chetu.”
Soma Pia: Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Hayo yamesemwa na Mhe. Wakili LEONARD TUNGARAZA MANYAMA ambaye ni Diwani wa Kata ya Wazo, Manispaa Ya Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam.
Mhe. Wakili Manyama amewasihi sana wanaCCM kudumisha umoja na mshikamano hasa wakati huu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili CCM iweze kushinda kwa kishindo.
Diwani Manyama ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Wazee na WanaCCM wa Tawi la Mivumoni, Kata ya Wazo, Wilaya ya Kinondoni.